08/08/2017
RIPOTI YA MWAKA MMOJA TOKA KUANZISHWA BARAZA LA VIJANA LA WILAYA YA MJINI.
UTANGULIZI;
Baraza la Vijana ni Taasisi yenye kujitegemea iliyoanzishwa kwa mujibu wa Sheria nambari 16/2013 iliyopitishwa na kutiwa saini na Mh. rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein
Baraza la Vijana ni chimbuko la Sera ya maendeleo ya Vijana ambayo iliandikwa na wadau baada ya kuona uwakilishi wa Vijana katika masuala yanayowahusu Vijana uzingatiaji na ushiriki ni mdogo.
Hivyo basi hadi mwaka 2013 ilianzishwa rasmi sheria ya Mabaraza ya Vijana na kupitishwa ndani ya Baraza la Wawakilishi chini ya Uongozi wa Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk: Ali Mohammed Shein ambaye aliatia saini Sheria ya uwanzishwaji wa Mabaraza hayo Sheria No 16 ya mwaka 2013
Mabaraza yameanzishwa kwa malengo yafuatayo:-
• Kuwajenga viajna kutambua utaifa wao ili kuongeza uzalendo na imani ya kuipenda nchi yao.
• Kuwa kiungo wakilishi na jukwaa la kutetea na kulinda maslahi ya vijana nchini.
• Kkushajihisha kujengewa uwezo kwa vijana ili kuwa wajenzi imara wa taifa na jamii .
• Kuwakilisha maslahi ndani ya vijana na nje ya nchi
• Kuongeza ushiriki wa vijana katika ngazi mbalimbali za maamuzi na katika ngazi za kiongozi.
Mchakato wa uhamasishaji ulianza mwaka 2014 ambapo takribani ya vijana elfu 2000 walifikiwa katika shehia zote za wilaya mjini, hatimae kuanza hatua nyengine kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa mabaraza kwa ngazi mbali mbali ngazi ya shehia na Wilaya.
Katika ngazi ya Shehia nafasi zilizogombaniwa ni:-
• Mwenyekiti
• Makamo Mwenyekiti
• Katibu
• Wajumbe 9 wa k**ati tendaji
Katika ngazi ya Wilaya nafasi zilizogombaniwa ni:-
• Mwenyekiti
• Makamo mwenyekiti
• Wajumbe 7 wa k**ati tendaji
Baraza la Vijana Wilaya ya Mjini lina jumla ya wajumbe 55 ambao ni wenyeviti wa mabaraza shehia
Baraza la vijana wilaya ya mjini linaundwa na wanachama wapatao 1860 wavulana 740 na wasichana 1120 kutoka shehia 55 zilizomo ndani ya wilaya ya mjini.
1. MAFANIKIO
Miongoni mwa mafanikio hayo ni k**a ifuatavyo:-
Kupatiwa kwa mafunzo kwa wanachama wa baraza
• Uongozi – uendeshaji wa Baraza na namna kuendeleza Taasisi, jumla ya Vijana wapatao 900 walipatiwa Mafunzo ya Uongo ambayo yalidhainiwa na Eqwips Hubs
• Ujasiriamali- Utengenezaji wa Sabuni,Shampoo,Taiz , Vijana 72 walipatiwa Mafunzo. ambapo jumla ya Vijana kumi na tano ( 15) wasichana walipatiwa Mafunzo jinsi ya kutengeneza mbolea za asili, kutengeneza mizinga ya Nyuki, kutengeneza dawa za asili bila ya kutumia kemikali, jinsi ya kutayarisha shamba na mbinu mbali mbali za kujikwamua kiuchumi.
• Kilimo :Mafunzo haya yalifanyika chini ya udhamini mradi wa Fursa kijani na Milele foundation, ambayo katika mafunzo hayo vijana watano wameweza kupatiwa Ajira.
• Sanaa na Ubunifu
• Uzalendo
• Kupiga kura
• Sheria
• Stadi za maisha takriban 100 walipatiwa Elimu za stadi za maisha ili kuweza kujitambua na kuepukana na changamoto za kundi rika ambazo hukabiliana nazo kila siku.
• Ukomavu wa kifedha (Eqwip hub)
• Utalii Jumla ya Vijana 10 waliweza kupatiwa Mafunzo ya Hotelia ambayo Mafunzo hayo yaliandaliwa na ILO na ZITOD kwa kushirikiana na Wizara ya kazi Zanzibar kwa lengo la kuinua fursa za vijana wa Zanzibar.
FURSA ZA AJIRA
• Kuajiriwa na vikosi mbali mbali – JKU na vikosi vyengine.
• Mahotelini
• Kujiajiri
• Takriban Vijana 43 wameajiriwa na waliojiri kupitia fursa mbali mbali ni Vijana 15.
• Uandishi wa miradi
• Mradi wa Chaki
• Jiwe Jeusi
• Uwezeshaji kiuchumi
• Taka ngumu na laini ( recycling process)
• Ufugaji wa kuku
• Kukuzamichezo na utamaduni
• Elimu ya lugha ya kiingereza
• Utumiaji sahihi wa rasilimali
2. USHIRIKI NA USHIRIKISHWAJI
Katika suala la ushiriki na ushirikishwaji limeongezeka kwa takriban asilimia 60% kitu ambacho kimeweza kufikia malengo ya uanzishwaji wa mabaraza ya Vijana .
Hili limeonekana katika kipindi cha mwaka mmoja kupitia Ushiriki na Ushirikishwaji wa Vijana kupitia Serikali na Sekta binafsi k**a ifuatavyo:-
• Utungaji wa Sera k**a ya Vijana,Uchumi na Afya
• Uandaaji wa mipango kazi na mikakati k**a vile wa tume ya Ukimwai Zanzibar
• Kongamano za kiutamaduni k**a vile Zanzibar International Film Festival (ZIFF)
• Udhibiti juu ya mipango ya Madawa ya kulevya.
• Kampeni za kusaidia Jamii k**a Mimi Na Wewe na Kijana paza sauti.
• Uandaaji wa Nakala na Vipeperushi mbali mbali vinavyohusu Vijana
• Ushiriki wa siku za maadhimisho mbali mbali za Kimataifa k**a vile siku ya mtoto Njiti ,mabaharia,madawa ya kulevya,ukimwi nk.
Baraza la Vijan wilaya ya Mjini limesaidia kuhamasisha Vijana katika kuzitambua na kuzifikia fursa zinazo walenga moja kwa moja mfano bahari, bahari ikitumiwa vizuri inaweza ikawa ni sehemu kubwa ya kuondoa tatizo la Ajira kwa Vijana wetu, pia taka ngumu, ambazo taka hizo baada ya kuzisanifu kutoka katika uhalisia wake na kuweza kukifanya kitu kipya ambacho kinaweza kikatumika katika maisha ya kiujumla, Ardhi katika matumizi ya kilimo k**a tujuavyo kwamba ardhi ndio uti wa mgongo wa taifa letu, hivyo Vijana wetu wakiitumia vidhuri ardhi hii kwa kilimo cha kisasa itawatoa katika moja na kuwapeleka hatua nyengine
3. MAHUSIANO NA TAASISI MBALIMBALI
EQWIPHUB ZAFAYCO
MICHAEL JOHNSON MYDO
UNFPA VSO
SAMBA FOUNDATION ZURA
TASAF JABAL NOR
ZACA ZAC
CYD ZLSC
ZYF ZAYEDESA
SYPC MELISHA
SERIKALI
• Ofisi ya Makamo wa pili wa Rais
• Wizzara inayohusiana na masuala ya vijana
• Wizara ya habari
• Wizara ya afya
• Wizara tawala za mikoa
• Ofisi ya mkuu wa mkoa
• Ofisi ya mkuu wa wilaya
4. CHANGAMOTO.
Licha ya Mafanikio hayo yote kipindi cha mwaka mmoja kilikua ni kipindi kikubwa cha kujifunza na kujipanga imara katika kuhakikisha dhana nzima ya Baraza la Vijana Wilaya ya Mjini yanafikiwa sambamba na malengo ya uanzishwaji wa baraza la vijana Zanzibar.
Hivyo baraza la vijana lilikumbana na miongoni mwa changamoto ambazo zinahitaji kufanyiwa kazi kwa pamoja na kushirikiana na baraza la wilaya ya mjini’
Miongoni mwa changamoto hizo ni k**a ifuatavyo:
• Kutojuulikana lengo kuu la Baraza la Vijana
• Kutoungwa mkono na baadhi ya taasisi za kiserikali na binafsi
• Dhana nzima ya kujitolea na utetezi.
• Kutokuwepo kwa bahshish kwa viongozi wa Mabaraza
• Uhaba wa vitendea kazi k**a kamera ,laptop,desktop na projector
• Ukosekanaji wa miundo mbinu ya kutendea kazi
• Uelewa mdogo juu ya dhana nzima ya uongozi
• Uwepo wa muhali kwa viongozi wa juu katika kuchukua hatua juu ya kulinda haki za vijana na kuskilzwa k**a sheria inavyoelekeza.
5. MAPENDEKEZO
• Serikali kuongeza mbinu za ufanisi katika kuhakikisha vijana wanaendelea kupewa kipaumbele nchini kupitia mabaraza hususan fursa zinazowahusu vijana.
• Serikali kuondoa sheria au kuzirekebisha ili kuhakikisha maslahi ya vijana yanafikiwa k**a malengo ya uanzishwaji yalivyo. Mfano udhalishaji na unyanyasaji,baraza la vijana baadhi ya vifungu nk.
• Sekta binafsi kuwapa vipaumbele vijana kupitia Baraza la vijana wilaya mjini juu ya fursa zilizopo.
• Vijana kujiunga na kuibeba dhana ya kujitolea k**a sehemu ya kujipatia uzoefu na kuongeza network na wadau mbalimbali ili kufikia malengo yao .
HITIMISHO
Shukrani zetu za dhati kabisa zimuendee mh Raisi wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baaza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein kwa kutuletea chombo ambacho kina mnasaba wa kuunganisha sauti za vijana ili kujitetea na kusaidia taifa katika kutatua changamoto zao na taifa kwa ujumla.
Pili kuishukuru wizara ianyohusiana na masuala ya vijana,
Ofisi ya mkuu wa mkoa wa mjini mgahribi kwa mchango mkubwa na kuwa sambamba na vijana bega kwa bega.
Ofisi ya mkuu wa wilaya ambayo imekua bega kwa bega kushirikiana nasi kwa kila jambo tunalifanya basi mkono wa fisi hii uko ,hongera zifikie hususani kwa mkuu wa wilaya ya mjini.
Bila ya kuwasahu wadau mbalimbali k**a vile eqwiphub ,mydo,Zanzibar youth council na wadau mbalimbali ambao wengine wapo nasi hapa hii leo.
MUELEKEO WABAADAE
• Baraza la Vijana wilaya ya Mjini kua ni Chombo cha mabadiliko chanya katika jamii
• Kuwa ni sehemu ya utetezi wa masuala ya vijana nchini
• Kuongeza wanachama ili kuwa na sauti yenye nguvu nay a kusikika ili kufikia malengo yake.