Michezo NA Burudani

Michezo NA Burudani Wadau wote wa soka karib tuburudike sports kwanza mambo mengine baadae

01/02/2023
15/05/2020

Mkataba wa David Silva, 34, kwa Manchester City unakamilika Juni 30 lakini Mhispania huyo anayecheza safu ya kati,yuko tayari kuongeza mkataba huo hadi mwisho wa msimu, kabla ya kufunganya virago

15/05/2020

TETESI ZA SOKA: JUVENTUS INATAKA KUMCHUKUA JORGINHO NA KUWAPA CHELSEA PJANIC

- Inadaiwa Kocha wa Juventus, Maurizio Sarri ana shahuku ya kufanya kazi na Jorginho kwa mara nyingine baada ya kuhama naye kutoka Napoli kwenda Chelsea mwaka 2018

- Sarri aliondoka Chelsea na kumuacha Jorginho na sasa Juventus inadaiwa kuwa tayari kumuongeza Pjanic aliyebakiwa na mwaka mmoja kwenye mkataba wake ili wamnase Jorginho

Je, unadhani timu gani itakuwa imepata faida iwapo uhamisho huu utafanikiwa?

07/05/2020

Msimu wa ligi ya Ujerumani-Bundesliga utaanza tena Mei 16, kwa kuchezwa pasipo mashabiki uwanjani, ikiwa ni takribani miezi miwili tangu usimamishwe kutokana na janga la virusi vya corona. Tangazo hilo la leo limetolewa baada ya vilabu vya kandanda kuambiwa msimu unaweza kuanza kutokana na mkutano wa Kansela Angela Merkel na viongozi wa majimbo 16 ya Ujerumani. Mkurugenzi Mtendaji wa Ligi ya Soka ya Ujerumani Christian Seifert amesema uamuzi huo una maanisha uhai wa uchumi wa vilabu, na kwamba kila mtu anapaswa kuwa macho kabisa kwamba ni michezo ya majaribio na kusisitiza kila mmoja kusimamia vyema majukumuku yake. Siku ya mwazo Jumamosi ya Mei 16 mchuano huo utazikutanisha timu 12 ambapo Borussia Dortmund itafuana na Schalke, Leipzig na Freiburg, Hoffenheim na Hertha Berlin, Dusseldorf na Paderborn na Augsburg na Wolfsburg.

04/05/2020
03/05/2020

REAL MADRID YAANDAA KITITA KUMNASA POGBA

Real Madrid inaandaa kiasi cha pauni milioni 70 ili kumsajili kiungo wa Manchester United, Paul Pogba (27).

Kiungo huyo raia wa Ufaransa, tayari amekwishaiarifu timu yake ya Man United kuwa hatasaini mkataba mpya mara mkataba wa sasa utakapomalizika mwaka mmoja ujao, akitaka kutafuta maisha sehemu nyingine.

PSG ambao ndiyo wapinzani wakubwa wa Real Madrid katika kinyang’anyiro cha kumuwania kiungo huyo, tayari walishanyoosha mikono na Pogba mwenyewe amekuwa akionesha dalili za kuchagua soka la Hispania kuliko sehemu nyingine.

Miaka minne iliyopita, Pogba alisajiliwa na United kwa dau la pauni milioni 89 na mkataba wake umebakiza mwaka mmoja.

Je, aende Real Madrid au abaki man United?

Address

Kigombe
Tanga

Telephone

+255716415084

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Michezo NA Burudani posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category