Dimba zone.

Dimba zone. Habarika Ki Michezo na Burudani,Kitaifa na Anga la Kimataifa.

12/01/2019

Kila la kheri Simba SC wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika.

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, inatarajiwa kuondoka ijumaa ya Novemba 16 mwaka huu kwenda nchini Lesotho  kwaaji...
13/11/2018

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, inatarajiwa kuondoka ijumaa ya Novemba 16 mwaka huu kwenda nchini Lesotho kwaajili ya kucheza mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya AFCON 2019 Nchini Cameroon.

Stars ambayo ipo kambini nchini Afrika ya kusini itaondoka kwa basi kwenda Lesotho wakati mchezo ukitarajiwa kuchezwa siku ya Jumapili ya Novemba 18 mwaka huu.

Carabao Cup 21:45
26/09/2018

Carabao Cup 21:45

Kabla ya dirisha la usajili kufungwa nchini Uingereza siku ya alhamisi, swali la kujiuliza ni kwamba !!! Je, Allison ata...
07/08/2018

Kabla ya dirisha la usajili kufungwa nchini Uingereza siku ya alhamisi, swali la kujiuliza ni kwamba !!! Je, Allison ataendelea kushikilia rekodi ya kuwa kipa ghali zaidi duniani kwa sasa, au Arrizabalaga atavunja rekodi ya Allison anayoishikilia hadi sasa baada ya kusajiliwa na Liverpool kutoka AS Roma kwa £35m.

Ikumbukwe kuwa Real Madrid tayari wametoa offer ya £35m pia kwa Chelsea ili kumpata Thibout Courtois na Chelsea wanahaha kumpata mbadala wa Courtois.

Athletic Bilbao wao wamesema endapo Chelsea wanamtaka kipa wao Kepa Arrizabalaga basi watoe kiasi cha £72m.

Na taarifa zinasema kuwa Chelsea wamekubali kutoa pesa hiyo.

K**a mambo yakiwa hivi basi Arrizabalaga atakuwa ndiye kipa ghali zaidi kuwahi kutokea duniani.

14/05/2018

Nawashukuru wote Mlio like page hii na wote Mnaondelea kulike page hii, si muda mrefu Jambo zuri litakuja kwako....

Habarika Ki Michezo na Burudani,Kitaifa na Anga la Kimataifa.

Ratiba kamili robo fainali;Europa league leo:-CSKA Moscow Vs Arsenal22:05RB Salzburg Vs Lazio22:05Marseille Vs RB Leipzi...
12/04/2018

Ratiba kamili robo fainali;

Europa league leo:-

CSKA Moscow Vs Arsenal
22:05

RB Salzburg Vs Lazio
22:05

Marseille Vs RB Leipzig
22:05

Sporting Vs Atl Madrid
22:05

Mshambuliaji wa Tottenham na timu ya taifa ya Uingereza Harry Kane sasa apewa rasmi goli lililokuwa na utata.Goli la pil...
12/04/2018

Mshambuliaji wa Tottenham na timu ya taifa ya Uingereza Harry Kane sasa apewa rasmi goli lililokuwa na utata.

Goli la pili la Tottenham dhidi ya Stoke city katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza awali alipewa kiungo wa kati wa timu hiyo Christian Eriksen kutokana na free kick aliyopiga kwenye mchezo huo.

Wasimamizi wa ligi kuu ya Uingereza wamesema mpira wa mwisho ulimgonga Kane kwenye bega kabla ya kubadili uelekeo na kuingia nyavuni.

Katika mchezo huo uliopigwa tarehe 7 Aprili ulimalizika kwa Spurs kushinda kwa magoli 2 kwa 1.

Kwa upande wake Harry Kane alisema hakuwa na shida yoyote katika maamuzi ya awali ambapo goli hilo alipewa mchezaji mwenzake Christian Eriksen, na kusema kuwa anacho shukuru ni kwamba timu yake imepata ushindi.

Kwa maamuzi hayo sasa Harry Kane anafikisha jumla ya magoli 25 na kuwa nyuma magoli 4 dhidi ya kinara wa magoli katika ligi hiyo kwa sasa mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah mwenye jumla ya magoli 29.

Ligi kuu Tanzania bara inaendelea leo kwa mchezo mmoja utakao pigwa katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam.Simba spo...
12/04/2018

Ligi kuu Tanzania bara inaendelea leo kwa mchezo mmoja utakao pigwa katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam.

Simba sports club itakuwa mwenyeji wa Mbeya City matajiri kutoka jijini Mbeya.

Kutokana na matokeo ya jana ambapo Yanga sports club walitoka sare ya goli 1-1 dhidi ya Singida United yanaipa Simba nafasi ya kuzidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Tanzania bara.

12/04/2018

Kutoka BBC Swahili;
Jumapili hii mji wa Gold Coast Australia utaukabidhi kijiti cha uenyeji wa michezo ya jumuiya ya madola mji wa Birmingham wa Uingereza.
Birmingham inategemea kuwa mwenyeji wa michuano ya jumuiya ya madola ya mwaka 2022.
Mpango wa paundi milioni 70 kukipanua na kukiboresha Alexander Stadium ya Birmingam umetangazwa.Mpango huo utakiboresha kiwanja hicho chenye umri wa Zaidi ya miaka 40 kutoka kuweza kubeba watu 12,700 mpaka watu 40,000.
Tayari picha ya namna kiwanja hicho kinavyotarajiwa kuonekana imewekwa wazi na iwapo mpango utasalia ulivyo basi nchi nyingi zitaweza kuziona rangi za bendera zao kwani paa la Uwanja huo litakuwa na mifuniko ambayo ina rangi za bendera za nchi kadhaa Duniani.
Upanuzi huu utakifanya pia kiwanja hiki kuwa kikubwa zaidi chenye uwezo wa kutumika kwa michezo mbalimbali ya riadha, ukiacha vile vilivyoko London.

08/03/2018

Address

Nurdinamran@gmail. Com
Tanga
0404012

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Dimba zone. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Dimba zone.:

Share

Category