11/10/2022
CAF WATOA ONYO KWA AL HILAL
Klabu ya Al Hilal imepewa onyo kutoka shirikisho la mpira wa miguu Afrika CAF kuwa wawe makini na mashabiki wao katika mechi za klabu bingwa dhidi ya vitendo vya vurugu uwanjani pale Hilal wanapokuwa nyumbani.
Hili limekuja baada ya mashabiki kufanya vurugu na kuonyesha tabia zisizokuwa za kimpira katika mchezo wa kwanza wa Al Hilal dhidi ya St.George baada ya Hilal kufunga goli na kufanikiwa kufuzu hatua hii ya pili.
Ikiwa Al Hilal watashindwa kutimiza onyo hilo watakutana na adhabu ya faini au kufungiwa kushiriki michuano hiyo kwa mujibu wa kanuni na sheria za uendeshaji wa michezo inayosimamiwa na shirikisho hilo la mpira Afrika.
✍️Middlecharz Sports INFO
🔎Mickyjnr