06/04/2026
Achana na porojo za walioshindwa.. Simba timu yao ni mbovu sana, wanapo shindwa kutimiza walicho tegemea huja na vimakosa vya kijinga.. Leo hii kilicho waangusha ni wachezaji hao hasa Geye na Mwenzake Aura.. Jamaa ni wachoyo sana, Wana mambo mengi ambayo kimpira hasa mechi ngumu hutakiwi kufanya. Kila mmoja anataka kuonyesha kuwa yeye ni fundi wa boli, hawako tayari kucheza kimkakati ili kuisaidia timu.
Mashabiki kazi yao ni kuja kulialia bila kuangalia majukumu ya hovyo wanayo fanya wachezaji wao.
Binafsi lawama anazopewa refa ni kutafuta kichaka cha kujificha kwa ubovu wa timu yenu.. Na nivile mmekutana Azam naye kiazi kwa sababu nafasi k**a ile ya Sadun unakosaje kufunga? Yote tisa.. Kumi. Arajiga ni tunu ya Taifa kwa marefa hapa Tanzania.. Anatakiwa kulindwa, k**a binadamu anamakosa yake lakini kwa leo amechezesha vizuri bila wasi Wasi wowote.
Mkianza milio ya marefa itakuwa ni dalili ya kushindwa coz badala mjikite kutengeneza timu, nyie mko bize kutaka ubingwa wa Email.