Soka & Udaku

Soka & Udaku Karibu Kwenye Page Yetu ya SOKA na Udaku Kwa Taarifa za MICHEZO (tetesi za usajili)Udaku Trending str

✍️ Anaandika Feisal Salum Ndugu zangu Watanzania;Kwanza namshukuru Allah kwa kila jambo, kwa utulivu wa nafsi na namna a...
09/06/2023

✍️ Anaandika Feisal Salum

Ndugu zangu Watanzania;

Kwanza namshukuru Allah kwa kila jambo, kwa utulivu wa nafsi na namna alivyonijalia hadi muda huu nikiwa mchezaji wa Azam Fc.
Namshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia kwa namna ya kipekee na namna anavyofuatilia michezo na kutulea sisi watoto wake. Binafsi sina la kumlipa zaidi ya kuifia jezi ya Timu ya Taifa ya Tanzania.
Nawashukuru Watanzania wote kwa mapenzi yao kwangu, nawashukuru Mashabiki wa Yanga na uongozi kwa miaka yote tulokua pamoja, haikua rahisi mimi kuondoka.
Kipekee niwashukuru wachezaji wote nilocheza na Yanga na kufurahia michezo mingi ya ushindi na kumbukumbu nyingi pamoja. Hatukuwa tu wachezaji wa timu moja bali familia.
Niwashukuru Azam Fc kwa kuona nafaa kucheza timu hii na nawaahidi ubora na jasho la kweli kutafuta mafanikio. Kwangu mimi hii ni klabu kubwa yenye hadhi ya mimi kuichezea.
Maisha mapya yameanza, tuvae jezi namba 6 ya na tujae kwenye michezo yetu, nyakati mpya zimeanza.
✍️

Feisal Update 🚨 YYoung Africans Sports ClubAYoung Africans Sports ClubSYoung Africans Sports ClubClub to AAzam FCFCHapo ...
08/06/2023

Feisal Update 🚨
YYoung Africans Sports ClubAYoung Africans Sports ClubSYoung Africans Sports ClubClub to AAzam FCFC
Hapo vipi wazee😁

🚨Habari kwisha! N'Golo Kanté ataungana na  Karim Benzema ndani ya klabu ya Al-Ittihad. 🇸🇦 N’Golo KANTE tayari amekubali ...
07/06/2023

🚨Habari kwisha! N'Golo Kanté ataungana na Karim Benzema ndani ya klabu ya Al-Ittihad. 🇸🇦

N’Golo KANTE tayari amekubali kujiunga Na klabu ya Ittihad huku mashabiki wa soka wakimshambulia kwenye mitandao yake ya kijamii kua ameharibu mustakabali wa maisha yake ya soka kwa kufuata pesa

Ikumbukwe kua Kanté atapokea Euro milioni 100 hadi mwezi juni mwaka 2025 .

(SOURCE: Fabrizio Romano)

Vp mdau N’Golo Kanté unamuunga mkono au ameharibu ? Toa maoni yako 😁😁😁
MagingMaginger Soka️

RASMI : Karim Benzema amejiunga na Al-Ittihad kwa kandarasi ya miaka mitatu. 🇸🇦✍🏻
06/06/2023

RASMI : Karim Benzema amejiunga na Al-Ittihad kwa kandarasi ya miaka mitatu. 🇸🇦✍🏻

ZA HIVI PUNDE🔸Kiungo wa Yanga Feisal Salum "Fei toto" muda huu yupo njiani kwenda makao makuu ya Yanga kukutana na CEO w...
06/06/2023

ZA HIVI PUNDE🔸Kiungo wa Yanga Feisal Salum "Fei toto" muda huu yupo njiani kwenda makao makuu ya Yanga kukutana na CEO wa timu hiyo kwa ajili ya kikao cha kujua mustakabali wake,rais wa Yanga si sehemu ya kikao hicho.

Hiii imetokana Na ombi la jana la Muheshimiwa rais mama Samia Suluhu Hassan kuwaomba viongozi wa Yanga wamalize ugomvi uliopo kati yao Na mchezaji huyo

MMaginger SokaSoka✍️

  : K**a utakuwa ni moja kati ya watu ambao wanandoto siku moja kuja kumiliki magari ya kifahari basi leo kwa uchache tu...
06/06/2023

: K**a utakuwa ni moja kati ya watu ambao wanandoto siku moja kuja kumiliki magari ya kifahari basi leo kwa uchache tunakufahamisha gharama za kubadilisha oil kwa magari baadhi ya kifahari.

Kupitia mtandao wa Bugatti Browad unaandika gharama za kubadili oil kwa magari hayo ni kuanzia Million 47,340,000 hadi Million 59,175,000 na kutofautia huku inategemeana na modeli ya Bugatti husika, na wauzaji wa magari haya pia wanashauri walau oil ibadilishwe mara moja kwa mwaka.

Mtandao wa J.D. Power unataja gharama za kubadili oil kwenye gari aina ya Lamborghini ni Kuanzia Laki 946,800 hadi Million 4,734,000 kwa kutegemeana na modeli ya Lamborghini husika, na inashauriwa kubadilishwa kwa kila baada ya Miles 9,000 ambayo ni sawa na Kilomita 14,484.

Mtandao wa Rolls-Royce Motor Car unataja gharama za kubadilisha oil kwenye gari hizo ni kuanzia Millioni 1,538,550 hadi Millioni 4,734,000 na hii pia inategemeana na modeli ya gari na mwaka husika, Kwa kawaida pia wameshauri kubadilishwa kwa oil wa gari hiyo kuanzia Kilomita 4,828 hadi 11,265 ambayo ni sawa na mara mbili hadi moja kwa mwaka.

Kwa upande wako unatumia muda gani kubadilisha oil ya gari yako? na huwa inakugharimu kiasi gani?

📝:

&udaku

Address

Mbeya

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Soka & Udaku posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category