Fedoh

Fedoh Habari moto za soka la Bongo na Dunia!
⚽️ Usajili, magoli,
🎯 Tunachambua kandanda kwa mitazamo 360° – bila kupendelea!

04/04/2026

BABU KAJU 🙌🏽🔥kaokota nae leo... mtag shabiki wa simba sc

29/03/2026

Taifa Satrs wanaendelea kugawa Dozi kwa Macau,kipindi cha Kwanza wamewapoga Goli 3:0 (MMombwa,mwamnyeto na Mudathiri)

Ikiwa ni mchezo wa kutafuta mshindi wa Tatu leo.
gonga like k**a umecheki game leo!....

28/03/2026

Sasa unaweza kusema vita mke ya Sheria kati ya Senegal na Caf inaendelea,⤵️⤵️⤵️

Nawaandikia ujumbe huu nikiwa na machozi ya furaha na shukrani machoni mwangu. Kwangu ninyi si mashabiki tu, bali ni fam...
28/03/2026

Nawaandikia ujumbe huu nikiwa na machozi ya furaha na shukrani machoni mwangu. Kwangu ninyi si mashabiki tu, bali ni familia bora zaidi ambayo nimewahi kukutana nayo duniani.

Nataka kuwashukuru kwa dhati ya moyo wangu kwa msaada wenu usioyumba. Hata katika nyakati ngumu na za giza ambazo nimepitia, hamkuniacha.

Mliendelea kuniamini, mkanishika mkono, na kunipa nguvu ya kusimama tena kutokana na Maombi yenu yasiyokoma, Simu na ujumbe wenu wa upendo na ushauri wenu wa dhati ndiyo maana leo ninaanza kurudi kwenye mstari wangu wa mafanikio.

Upendo wenu umenifanya niamue jambo moja: Sitawasaliti. Nimeamua kuendelea kubaki na kupambana ndani ya klabu hii ninayoipenda.

Ninawapenda sana na ninaahidi kuwapa furaha na mambo mema zaidi katika siku zijazo. Safari yetu bado inaendelea!

SIMBA NGUVU MOJA!
UBAYA UBWELA! 🔥 🔥 🔥

Klabu ya Simba SC imekumbwa na rungu lingine la kinidhamu baada ya kutozwa faini ya Shilingi Milioni 10 kufuatia kitendo...
27/03/2026

Klabu ya Simba SC imekumbwa na rungu lingine la kinidhamu baada ya kutozwa faini ya Shilingi Milioni 10 kufuatia kitendo cha mashabiki wake kuwarushia chupa za maji waamuzi katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Pamba Jiji. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mwandishi Felix Jason, adhabu hiyo imekuja baada ya kubainika kuwa hili ni kosa linalojirudia ndani ya kipindi cha miezi miwili tu, ambapo awali mashabiki hao walifanya kitendo k**a hicho katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji.

​Hali hii ya utovu wa nidhamu inazidi kuingia gharama klabu hiyo ya Msimbazi, huku k**ati za nidhamu zikionekana kutofumbia macho vitendo vinavyoharibu taswira ya soka la Tanzania. Wakati uongozi wa Simba ukiendelea kutoa rai kwa mashabiki wake kudhibiti hisia zao uwanjani, adhabu hii inatumika k**a onyo kali kuwa makosa yanayojirudia yanaweza kuzaa adhabu nzito zaidi, ikiwemo kucheza michezo bila mashabiki au kupoteza pointi muhimu, jambo ambalo linaweza kuvuruga mbio za ubingwa msimu huu.

Unadhani kuna umhimu wa mashabiki sasa kuichangia simba sc?

Mlinda mlango namba moja wa Young Africans, Djigui Diarra, amekumbwa na rungu la kinidhamu baada ya kufungiwa kucheza mi...
27/03/2026

Mlinda mlango namba moja wa Young Africans, Djigui Diarra, amekumbwa na rungu la kinidhamu baada ya kufungiwa kucheza michezo mitatu (3) pamoja na kutozwa faini nzito ya jumla ya Shilingi Milioni Nne (4,000,000) kufuatia utovu wa nidhamu uwanjani.

Taarifa zinaeleza kuwa kipa huyo raia wa Mali ameadhibiwa kwa makosa mawili tofauti; kwanza ni kosa la kumshambulia mwamuzi ambalo limemgharimu faini ya Shilingi Milioni Mbili na kifungo cha mechi hizo tatu, na kosa la pili ni kuonyesha ishara isiyofaa (kidole cha kati) ambayo imemuongezea faini nyingine ya Shilingi Milioni Mbili.

Umeridhika na adhabu hii....?

Klabu ya Simba SC imeonyesha imani kubwa kwa kiungo wake mshambuliaji, Elie Mpanzu, baada ya kumsainisha mkataba mpya wa...
23/03/2026

Klabu ya Simba SC imeonyesha imani kubwa kwa kiungo wake mshambuliaji, Elie Mpanzu, baada ya kumsainisha mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuitumikia timu hiyo yenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam. Uamuzi huu unakuja wakati ambapo mchezaji huyo ameanza kuonyesha mchango wake ndani ya kikosi, licha ya takwimu ambazo bado zina nafasi ya kuimarika zaidi.

Mpanzu hadi sasa amecheza jumla ya mechi 13, akikusanya dakika 626 uwanjani. Katika kipindi hicho, amefanikiwa kufunga mabao 2 pamoja na kutoa pasi 5 za mabao (assist), jambo linaloonyesha kuwa anahusika moja kwa moja katika mafanikio ya timu anapopata nafasi ya kucheza.

Kwa mtazamo wangu kiufundi, takwimu hizi zinaashiria kuwa bado anaendelea kujizoesha mazingira ya ligi pamoja na mfumo wa uchezaji wa Simba. Hata hivyo, uwezo wake wa kutengeneza nafasi na kusaidia wachezaji wenzake kufunga unaonekana kuwa ni moja ya silaha muhimu kwa timu hiyo.

Uongozi wa Simba umevutiwa zaidi na uwezo wa muda mrefu wa mchezaji huyu kuliko takwimu za sasa pekee. Kusaini mkataba mpya ni ishara kwamba benchi la ufundi linaamini kuwa Mpanzu ana nafasi ya kuwa mchezaji muhimu zaidi katika misimu ijayo, endapo ataendelea kuimarika kimchezo na kuongeza ufanisi wake katika kufunga na kusaidia mabao.

Kwa upande wa mashabiki, usajili huu unaweza kupokelewa kwa mitazamo tofauti. Wapo watakaoona bado hajafikia kiwango cha juu kinachotarajiwa, huku wengine wakiamini kuwa ana uwezo mkubwa ambao haujaonekana kikamilifu kutokana na muda mdogo wa kucheza.

Kwa ujumla, uamuzi wa Simba SC kumpa mkataba mpya Elie Mpanzu ni uwekezaji wa kimkakati unaolenga kujenga kikosi chenye mwendelezo na kina cha kutosha. Sasa macho na masikio ya wengi yataelekezwa kwake ili kuona k**a ataweza kulipa imani hiyo kwa kuongeza kiwango chake na kuwa tegemeo kubwa zaidi ndani ya kikosi hicho.

23/03/2026

Msemaji wa TRA united Christina Mwagala amesema kila mmoja ashinde nyumbani kwake,Simba wameshinda Isamuyo lakini na wao watashinda Arusha nyumbani..

Unakubaliana na Kauli hii au atulie tu...?

23/03/2026

Golikipa wa Klabu ya Simba ambaye yupo nje ya Kikosi Akiuguza majeraha Pin Pin Camara akiwa na Mashabiki za zake baada ya Mchezo wa Timu yake dhidi ya TRA.

22/03/2026

"Uzuri wa Yanga Hata Wapinzani wetu nao wamevurugwa wanazidi kufanya Vibaya inatupa Nguvu sana"

22/03/2026

Leo Kujitutumua tunajitutumua na ushindi unapatikana!
Ukiangalia kwa umakini unaona penati au unaona k**a mimi?

Address

Makongo

Telephone

+255678663486

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Fedoh posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Fedoh:

Share

Category