04/11/2023
Kocha Mamelodi Sundowns, Rhulani Mokwena ameijia juu klabu ya Al Ahly kwa kile alichokitaja k**a "wanalalamikia kila kitu" baada ya Mafarao hao kudai kuwa mwamuzi aliwanyima penalti katika mchezo wa mkondo wa pili wa nusu fainali ya kombe la Afrika 'AFL'.
Al Ahly ilipoteza kwa matokeo ya jumla ya 1-0 kufuatia kipigo cha 1-0 katika dimba la Loftus Versfeld, Pretoria Afrika Kusini kabla ya sare ya 0-0 kwenye marudiano Cairo. Baada ya mechi hiyo Mafarao hao walimlalamikia Mwamuzi kuwa aliwanyima penalti.
βNashangazwa sana na Al Ahly wanalalamikia kila kitu. Kabla ya mechi ya kwanza, Al Ahly walilalamika kwamba tulicheza saa 9:00 alasiri na bado walikuwa na uwezo wa kurekebisha mchezo kwa wakati unaofaa wakiwa kwao, lakini hautasikia malalamiko kutoka kwa Sundowns."
βKinachoshangaza zaidi ni kwamba Al Ahly huwa wanalalamikia waamuzi pale tu wanapopoteza. Jose Mourinho aliwahi kusema kuwa klabu kubwa inapoanza kutafuta sababu nyingine nje ya soka inaposhindwa basi ndio inaanza kupoteza hadhi yake ya kuwa klabu kubwa. Natumai sivyo ilivyo kwa AL Ahly kwa sababu ni kielelezo cha soka la Afrika."
βBaada ya malalamiko hayo ni nini hasa lengo lao? Kwa sababu ninaweza kupitia orodha ya matukio, ambapo waamuzi hawakufanya kile nilichofikiri ni haki kwetu. Mwishoni mwa mechi, Sundowns ilifanya faulo saba na kupata kadi mbili za njano lakini Al Ahly walifanya faulo 13 na kupata kadi moja ya njano. Nadhani k**a kuna timu ilipaswa kulalamika basi ilitakwa kuwa Sundowns.β alieleza Mokwena.
Sundowns itachuana na Wydad Casablanca katika fainali ambapo mechi ya mkondo wa kwanza wa fainali itapigwa Jumapili Novemba 5, katika dimba Mohammed V, Casablanca kabla ya kurudiana Novemba 12, 2023 katika dimba la Loftus Versfeld, Pretoria Afrika Kusini.
Mshindi wa michuano hiyo mipya kabisa atatia kibindomi kitita cha dola milioni 4, huku mshindi wa pili akitarajiwa kuchukua dola milioni 3.