26/02/2016
MINENO YA JERRY YAMTOA POVU HAJI MANARA AAPA KWENDA POLISI.
Baada ya Simba SC kupigwa goli 2 - 0 hii ndo ilikuwa kauli ya Murro.
"Wamchangani hawawezi kutufunga Sisi hata wachezeshe wachezaji wao 40 pamoja na viongozi wao 10 tena yule mzee wa kachumbari ya miiba (Mr . Makofia) awemo lakini hawawezi kuifunga Yanga ikiwa na wachezaji 12 pamoja na mimi. .
"Mara ya kwanza tumewalamba mbili, ikaja tena tumewalamba mbili . . Jamani kuna kubahatisha hapa??uwezo wa Thaban Kamusoko ni sawa na uwezo wa wachezaji wao viungo watatu, siongei tu kuna takwimu hapa.
"Wao wanaajiri kocha wanaenda kumpokea kwenye basi la Simba Mtoto ama Raha leo pale Ubungo,Sisi Yanga Afrika kocha wetu anapanda ndege huko Uholanzi tunampokea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere. . Utawezaje kuwaweka kwenye mizania sawa?Lazima wajue kutofautisha kati ya tui na maziwa japo vyote vinafanana"Alimalizia Jerry Murro.
Baada ya kusikia hayo Haji Manara leo amemshutumu Murro kuwa ametoa kauli zenye kibaguzi na lazima ataenda kumshtaki sio TFF tena bali ni Polisi ama Mahakamani
Haya ndio majibu ya Muro
“Kwani ni uongo kusema kocha wao amekuja kwa basi na wetu amekuja kwa ndege? Si wamemsajili kutoka Coastal pale Tanga na wetu ni Mholanzi amekuja kwa ndege. K**a amaamini amedhalilishwa aende kwenye vyombo vya dola akashtaki,” alisema Muro.