27/05/2024
UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI CECAAF IMEANGUKA - MASHINDANO YA AFRIKA
Ni takribani miaka miwili nyuma Ukanda wa Afrika mashariki ulikuwa ni ukanda tishio katika mchezo wa Soka la walemavu katika Bara la Afrika na Dunia kwa ujumla. Ukanda huo ambao umesheheni vigogo wa mchezo huu barani Afrika wakiongozwa na Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda waliweza kiteka hisia za mashabiki na serikali zao kwa kufanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali ya kimataifa.
Takwimu zinaonesha kwamba Mashindano ya mwisho ya Afrika yaliyofanywa na moja ya nchi za ukanda huo (Tanzania) chini ya udhamini wa Rais wa nchi Mh. Samia Suluhu Hassan kwa zaidi ya Dola 250,000 = Tsh. Million 600+ ya mwaka 2021, Tanzania ilishika nafasi ya 4 kwa ubora Afrika, Kenya nafasi ya 6 kwa ubora huku Uganda ikishika nafasi ya 11 kati ya nafasi 11 za afrika. Ubora wa Tanzania ulifanya Tembo Warriors ikafuzu kwenda Kombe la Dunia katia ya 4 bora za Afrika.
Mwaka huu 2024, Mashindano ya Afrika yamefanyika tena nchini Misri na nchi za Afrika mashariki zimewakilishwa na Tanzania, Kenya, Uganda na Burundi. Mashindano ya mwaka huu yalikuwa na nafasi 7 za kufuzu kwenda kombe la Dunia mwaka 2026. Mpaka sasa nchi za Afrika Mashariki zimepata matokeo ya kuporomoka kwa kasi kubwa katika viwango vya Afrika, Tanzania ikishika nafasi ya 8 kutoka 4, Kenya ikishika nafasi ya 11 ktoka 6, Uganda akiendelwa kushikilia nafasi yake ya 10 na mgeni Burundi akishika nafasi ya mwisho ya 12. K**a ni kushika Daraja basi nchi za afrika mashariki 3 zinazoshika nafasi za mwisho zingeshuka daraja.
Jambo la kusikitisha zaidi ni nchi hizi kushindwa kufuzu kwenda kombe la dunia katika nafasi 7zilizotolewa wa Afrika, Tanzania iliyokuwa inategemewa katika ukanda huu imeshindwa kufuzu kwa wageni wa mashindano haya k**a vile Moroco, Algeria na Misri ambao wanashikiri kwa mara ya kwanza au mara ya pili. Tanzania ambayo imeshiriki mashindano haya kwa mara ya tatu na kugombea nafasi ya kufuzu kwa mara ya pili imeambulia patupu k**a ilivyo kwa majirani zake. Katika mechi tano alizo cheza Tembo Warriors, ameshinda mechi moja dhidi ya Sierra Leone na kupoteza mechi zingine zote (4). Hili pigo kubwa sana kwa ukanda wetu hasa ukizingatia ukanda huu umetoa Katibu Mkuu wa shirikisho Afrika Ndg. Peter Oloo (Kenya), mwenyekiti wa uchaguzi Afrika Ndg. Kitimbo Lawrence (Uganda) na Mgombea wa Uraisi wa Afrika katika uchaguzi uliopita Ndg. Peter Sarungi (Tanzania).
Natoa pole kwa vijana wetu walio pambana kwa jasho na damu ingawa wameshindwa kufikia malengo kutokana na sababu mbalimbali hasa za usimamizi, uongozi na wa mikakati katika kuchagiza mafanikio yao. Rudini nyumbani tujipange kwa miaka mingine, 2030 sio mbali tunaweza kujisahihisha na kurudi kwenye kiwango chetu.
Nitoe rai kwa wasimamizi na viongozi kupitia maneno machache, KARMA IS REAL.
Peter Leonard Sarungi