22/08/2017
TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO JUMANNE 22/08/2017.
1.BRADFORD ya Ligi Daraja La Kwanza England, imemsajili Beki wa kulia Luke Hendrie kwa mkopo kutoka Burnley mpaka January. ( ).
2.BARCELONA imekataa tamaa ya kumsajili Kiungo Mshambuliaji wa Liverpool, Phillipe Coutinho baada ya Miamba hao wa Anfield kusisitiza kuwa nyota huyo wa Brazil "hauzwi". ( ).
3.Klabu ya BRIGHTON imethibisha kumsajili Mshambuliaji wa Kimataifa kutoka Ghana, Raphael Dwamena kutoka klabu ya Fc Zurich hivyo atasafiri mpaka UK kwa ajili ya vipimo ili kuungana na klabu hiyo iliyopanda daraja Ligi Kuu England msimu huu. ( ).
4.MSHAMBULIAJI wa Fiorentina, Nikolas Kalinic yupo katika Viunga vya San Siro kwa ajili ya vipimo vya afya ili kujiunga kwa mkopo na wababe hao wa Milan. Nyota huyo wa Croatia anajiunga na Ac Milan kwa mkopo wa mwaka mmoja kwa dau la pauni €5m(£4.6m), na endapo atafanya vizuri atasajiliwa jumla kwa pauni €20m(£18.3). ( ).
5.KIUNGO wa Inter Milan, Geoffrey Kondogbia yupo mbioni kujiunga na Valencia kwa mkopo haijajulikana ni Mkopo wa muda gani. ( ).
6.KLABU ya Millwall ya Ligi daraja la kwanza England, imempeleka beki wake wa kati Kwa mkopo, Sid Nelson katika klabu ya Yeovil ya Daraja la pili nchini humo mpaka January. ( ).
7.KIUNGO kinda wa Kimataifa wa Algeria na Arsenal mwenye umri wa miaka 19, Ismael Benncer yupo mbioni kuondoka Arsenal ili kujiunga na Empoli ya Italia.( ).
8.KLABU ya Leed United ya Championship inataka kumsajili Mshambuliaji wa Middlesbrough, Rudy Gestede.( ).
9.PLYMOUTH ya Ligi Daraja la kwanza England inataka kumsajili Mshambuliaji wa Celtic, Nadir Ciftci kwa mkopo wa muda mrefu.( ).
10.STOKE CITY inamtaka beki wa Tottenham Hotspur, Kevin Wimmer. ( ).
11.KIUNGO wa Stoke City, Moha El Ouriach amekubali kujiunga na klabu ya Espanyol kwa mkataba wa muda mrefu. ( ).
12.MSHAMBULIAJI wa Leeds United, Chris Wood amejiunga na Burnley kwa mkataba wa miaka minne.( ).
13.MSHAMBULIAJI wa Southampton Sam Gallagher amekubali kujiunga na Birmingham City ya Championship kwa mkopo wa muda mrefu.( ).
14.MSHAMBULIAJI wa Everton, Oumar Niasse anafikiria kujiunga na Fenerbahce kwa mujibu wa tovuti ya ya nchini humo. Mshambuliaji huyo wa Senegal alijiunga na Everton January mwaka Jana kutoka Lokomotiv Moscow ya Urusi kwa pauni £13.5m kabla ya kutolewa kwa mkopo kwenda Hull City.
15.KOCHA WA ZAMANI wa England, Steve McClaren amepata kibali ya kuifundisha Klabu ya Maccabi Tel Aviv ya Nchini Israel.( ).
16.KIUNGO wa Real Madrid , Mateo Kovacic yupo tayari kujiunga na wababe wa Anfield, Liverpool endapo Phillipe Coutinho atatimkia Barcelona. ( ).
17.CHELSEA imeweka kiasi cha pauni £91m mezani ikitaka kumsajili Mshambuliaji wa Torino, Andrea Belotti.( ).
18.JUVENTUS & MANCHESTER UNITED zinapigana vikumbo kuiwania saini ya Kiungo Kinda wa Arsenal mwenye umri wa miaka 18, Marcus McGuane.Manchester City pia wapo kwenye vita hiyo.( ).
19.TOTTENHAM imetenga kiasi cha pauni £20m ili kumsajili Kiungo wa Everton, Ross Barkley. ( ).
20.MANCHESTER CITY itajaribu kwa mara ya mwisho kuwasajili mabeki wawili wa Kati, John Evans kutoka West Brom na Ben Gibson kutoka Middlesbrough kabla ya dirisha la usajili halijafungwa jumatano ya wiki ijayo .( ).
21.PARIS SAINT-GERMAIN imetenga kiasi cha pauni £200m ili kuwasajili mastaa wawili kwa mpigo kutoka Monaco, Kylian Mbappe na Fabinho ambapo kwenye pesa hiyo, Mbappe ataigharimu PSG pauni £128m huku Fabinho pauni £78m.Hata hivyo imeelezwa kuwa PSG itamtaka Mbappe kwa mkopo ili kuukwepa mkono wa FIFA katika harakati za kufuja pesa hasa baada ya kumsajili Mshambuliaji wa Barcelona, Neymar kwa pauni £200m.( ).
22.KIUNGO wa Juventus Claudio Marchisio ameomba kuondoka katika klabu hiyo ya Turin huku ikielezwa kuwa Bosi wa Chelsea, Antonio Conte anamnyatia Kiungo huyo wa Italia mwenye umri wa miaka 31.( ).
23.GALATASARAY ya Uturuki inamtaka beki wa,Arsenal, Kieran Gibbs.( ).
24.VALENCIA inamtaka Kiungo wa Manchester United, Andreas Perreira kwa mkopo wa muda mrefu.( ).
25.BAYERN MUNINCH inataka kumrudisha Ujerumani Mshambuliaji wa PSG, Julian Draxler huku Man United, Arsenal na Man City zikimtaka.( ).
26.KIUNGO wa OGCE Nice ya Ufaransa, Jean-Michael Seri amekubali mkataba wa miaka minne ili kujiunga na Barcelona. ( ).
27.MANCHESTER CITY, BURNLEY, WEST BROM na WEST HAM zinamgombea Mshambuliaji wa Kimataifa wa Ghana na Lorient ya Ufaransa, Abdul Majeed.Nyota huyo ana thamani ya pauni £12m.( ).
28.MSHAMBULIAJI kinda wa Arsenal, Chuba Akpom anatakiwa na Vilabu vya Leeds United na Celtic. ( ).
SIKU NJEMA KWA WOTE!!!!