Vitimbi vya soka

  • Home
  • Vitimbi vya soka

Vitimbi vya soka 💥SOTE TUFURAHI NA SOKA LETU

Whatsapp +255 676167186

💥HII KALIReal Madrid waliandaa shughuli ya kumpongeza mshindi wa Kombe la Dunia, Marc Cucurella, kabla ya mchezo wao wa ...
27/08/2026

💥HII KALI

Real Madrid waliandaa shughuli ya kumpongeza mshindi wa Kombe la Dunia, Marc Cucurella, kabla ya mchezo wao wa nyumbani dhidi ya Real Sociedad katika uwanja wa Santiago Bernabéu… 🤍🫶🏆🇪🇸⬇️

Kwa kawaida, mshindi wa Kombe la Dunia anaporejea klabuni kwake, timu ya nyumbani humuenzi mchezaji wao mbele ya mashabiki na kumruhusu kuonyesha kombe hilo. 🏆👏

Lakini Cucurella alitaka kitu tofauti. ❤️

Hakutaka kunyanyua kombe la Dunia peke yake mbele ya mashabiki wa Bernabéu. Aliomba Mikel Oyarzabal asimame pamoja naye- kwa sababu hakulishinda kombe hilo peke yake. Walilishinda kwa pamoja wakiwa na timu ya taifa ya Uhispania. 🇪🇸🏆

Oyarzabal alialikwa kuingia uwanjani, na mabingwa hao wawili wa Kombe la Dunia wakasimama bega kwa bega mbele ya umati wa Santiago Bernabéu. 🤍

Oyarzabal ni mchezaji wa Real Sociedad👏

Leo hii, wanaweza kuwa wapinzani katika ngazi ya klabu. Lakini daima watabaki kuwa wachezaji wenza waliofanikiwa kuwa Mabingwa wa Dunia kwa pamoja. 🌍🏆❤️

Uwanja wa Bernabéu uliwapa wote wawili heshima na kutambuliwa walikostahili. 👏

HESHIMA KWA YEYOTE ANAYESTAHILI HESHIMA. 🏆❤️🇪🇸

💥Ronaldo🇧🇷:Nilipokwenda kwenye majaribio ya soka huko Valqueire nikiwa mtoto, nilitaka kucheza k**a winga wa kulia. Laki...
27/08/2026

💥Ronaldo🇧🇷:

Nilipokwenda kwenye majaribio ya soka huko Valqueire nikiwa mtoto, nilitaka kucheza k**a winga wa kulia. Lakini niligundua kuwa kulikuwa na watoto wengine 15 wanaowania nafasi hiyo hiyo. Nilipotazama upande wa winga wa kushoto, nilikuta watoto wengine 15 wakigombea nafasi hiyo pia.

Hivyo, nilifikiria kucheza nafasi ya ulinzi, lakini kulikuwa na wachezaji wengi mno waliokuwa wakigombea nafasi hizo pia. Kisha nikaamua kujaribu kucheza k**a mshambuliaji, lakini nikagundua kuwa watoto 20 walikuwa wakigombea nafasi hiyo.

Nilipotazama upande wa makipa, niliona wachezaji wawili tu. Hivyo, nilimwambia kocha kuwa mimi ni kipa. Mpango wangu ulifanikiwa, na nikachaguliwa kuwa kipa wa timu hiyo.

Wiki moja baadaye, nilimwomba kocha anitazame nikicheza k**a mshambuliaji. Baada ya kunitazama, alisema, "Nafasi yako ni kwenye ushambuliaji, si golini."

Kuanzia siku hiyo, nilijihakikishia nafasi k**a mshambuliaji. Kocha hakuwahi kujua kwamba kuwa kipa ilikuwa ni mbinu yangu tu ya kufanikiwa kuingia kwenye timu. Sikuwa na nia yoyote ya kucheza k**a kipa hapo awali.

💥Hii inatufunza ili kufikia ndoto zako lazima ufanye kitu cha ziada tofauti na wengine.

Jack Grealish🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿:"Nilipokutana na Messi kwa mara ya kwanza, nilimwambia: 'Leo, wewe ni mchezaji bora wa soka ambaye ...
07/06/2026

Jack Grealish🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿:

"Nilipokutana na Messi kwa mara ya kwanza, nilimwambia: 'Leo, wewe ni mchezaji bora wa soka ambaye nimewahi kumuona maishani mwangu.' Alitabasamu na kunishika mkono, kisha wakati wa mapumziko nikamwambia: 'Leo, tafadhali njoo Manchester City ... Guardiola anatupigia kelele wakati wote, na daima anasema: Messi hakuwahi kusubiri mpaka nimwambie chakufanya! Ukija City, ataacha kunifokea .’”

Aliongeza:

“Messi alitabasamu na kuondoka zake, kisha Rodri akaja na kuniuliza: ‘Ulikuwa unamwambia nini?’ Nilimweleza kisa chote, naye akaangua kicheko kabla ya kuuliza: ‘Unaweza kuongea hata Kihispania?’ Nikasema: ‘Hapana.’ Kisha akajibu: ‘Mjinga wewe, Messi haelewi Kiingereza!’ Hapo ndipo nilipogundua Messi alikuwa amenichezea kabisa, kwa sababu hakuelewa hata neno moja!” 😂😂😂

💥Iniesta kuhusu Ronaldinho kuelekea El clasico:"Kabla ya mechi ya El Clasico dhidi ya Real Madrid, Ronaldinho alinipigia...
17/04/2026

💥Iniesta kuhusu Ronaldinho kuelekea El clasico:

"Kabla ya mechi ya El Clasico dhidi ya Real Madrid, Ronaldinho alinipigia simu usiku wa manane. Nilivyopokea simu akaniambia:

'Andres, najua ni saa 9 tisa usiku, lakini sina budi kukuambia kitu:
Andres nitaondoka mwezi wa sita, kaka yangu tumefikia makubaliano ya hali ya juu na Real Madrid, wametoa hela kubwa ambayo siwezi kukataa, wewe ni mdogo na unaweza kunielewa, lakini tafadhali usiseme chochote kwenye chumba cha kubadilishia nguo au kwa uongozi, usinisaliti, ninakuamini zaidi kuliko mtu mwingine yeyote, Andres.'

Sikulala usiku kucha, ukweli sikuweza kuelewa kwamba anatuacha vipi na kwenda timu nyingine, haswa kati ya timu zote kwanini achague mpinzani wetu mkuu Real Madrid ...😠

Siku ya El Clasico ilipofika katika chumba cha kubadilishia nguo cha Santiago Bernabeu, na tulipokuwa tukibadilisha nguo zetu, Ronaldinho alisimama na kuanza kusema:

'Jamani, leo tuna mchezo muhimu, tutacheza dhidi ya timu imara, lakini siku hizi nimegundua kuwa sisi ni k**a familia kubwa. Niliwapigia ninyi nyote usiku wa manane kusema kwamba ninaondoka mwezi wa sita, lakini hakuna hata mmoja wenu aliyetoa siri, Nitakuwa hapa kwa miaka mingi zaidi, na sasa twendeni uwanjani tukawafundishe soka hawa watu wa Madrid.'💪

kumbe ile Ilikuwa mbinu ya uhamasishaji, ambayo ilikuwa na lengo maalum kwa Ronaldinho. Baada ya kile kilichotokea, nilielewa kuwa tulikuwa tayari kufia ndani badala ya kusalitiana.

Katika mechi hiyo ya El Clasico alifunga mabao mawili, na uwanja mzima wa Santiago Bernabeu walisimama kumpigia makofi👏, huyo alikuwa Ronaldinho." 🔥

💥K**a uliwahi kusikia stori kuhusu Ronaldinho kupigiwa makofi na uwanja mzima hata mashabiki wa upinzani (Real Madrid) basi ndio ilikuwa mechi hiyo👏.

💥Wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza mwaka 2006 kati ya Chelsea na Reading, mlinda mlango wa Chelsea Petr Cech ali...
16/03/2026

💥Wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza mwaka 2006 kati ya Chelsea na Reading, mlinda mlango wa Chelsea Petr Cech alipata jeraha la kichwa kufuatia teke la kichwa la mchezaji wa Reading Stephen Hunt.

Carlo Cudicini ambaye alikuwa ni kipa namba mbili alitakiwa aingie lakini pia akaumia na hivyo John Terry alitoka kwenye nafasi ya beki na kwenda langoni katika dakika za mwisho za mchezo na akaisaidia Chelsea kushinda 1-0.

Baada ya tukio hilo, Cech alilazimika kuvaa vazi kichwani la kujikinga katika michezo iliyofuata.

Umewahi kupewa stori gani kuhusu vazi la kichwa la Peter Cech?😂😂

💥Luis Nani🇵🇹: "Siku moja, Alex Ferguson alituuliza k**a kuna mtu angeweza kumrudisha nyumbani baada ya mchezo dhidi ya F...
08/03/2026

💥Luis Nani🇵🇹:

"Siku moja, Alex Ferguson alituuliza k**a kuna mtu angeweza kumrudisha nyumbani baada ya mchezo dhidi ya Fulham. Nikasema: 'Mimi bosi, nitakupeleka nyumbani, bila wasiwasi!' Kisha kwenye huo mchezo ilikuwa 2-1, tukapata penati na nikamuomba Giggs aniruhusu nipige, akakubali ila nilivyopiga nikakosa penati ile😁

Fulham wakasawazisha na kufanya iwe 2-2 katika dakika ya 88... Baada ya mchezo k**a tulivyopanga nikamchukua Sir Alex Ferguson nyumbani lakini hakuzungumza namimi njia nzima." 😅

K**a wewe ungekuwa ndio Ferguson ungekuwa katika hali gani kwenye hilo gari la Luis Nani😂.

💥Mwaka 1978, Ajax walikuwa na mechi ya kumuaga Johan Cruyff, ambapo waliwakaribisha Bayern Munich. Baada ya mechi, Johan...
01/03/2026

💥Mwaka 1978, Ajax walikuwa na mechi ya kumuaga Johan Cruyff, ambapo waliwakaribisha Bayern Munich.

Baada ya mechi, Johan Cruyff alisema: "Bayern waliingia uwanjani k**a wapiganaji, kana kwamba wanacheza fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya. Ilikuwa ni aibu kubwa na dharau kabisa." 👀🔥

Bayern Munich walishinda 8 - 0🙌😂😂😂.

💥Orlando Pirates walikuwa wanaongoza 1-0 dhidi ya Baroka mpaka dakika za lala salama katika mchezo wa Ligi Kuu ya Absa y...
28/02/2026

💥Orlando Pirates walikuwa wanaongoza 1-0 dhidi ya Baroka mpaka dakika za lala salama katika mchezo wa Ligi Kuu ya Absa ya Afrika Kusini Novemba 2016.

Baroka walipata kona dakika ya 95 na kipa wa Baroka, Oscarine Masuluke, akasogea kushambulia na kuisaidia timu yake kupata bao la dakika za mwisho.

Masuluke alifunga bao la kusawazisha kwa kubinuka (Tikitaka) na kufanya matokeo kuwa 1-1.

Bao hilo lilimaliza la pili, nyuma ya bao la scorpion la Olivier Giroud, katika orodha ya Tuzo ya Puskas(Goli bora la mwaka duniani).🙌🙌🔥

💥Kamera zilikuwa zikiwanasa mara nyingi wakiishangilia kwa pamoja katika klabu ya Uturuki ya Fenerbahçe, na wakawa k**a ...
26/02/2026

💥Kamera zilikuwa zikiwanasa mara nyingi wakiishangilia kwa pamoja katika klabu ya Uturuki ya Fenerbahçe, na wakawa k**a moja ya kielelezo cha mapenzi ya kweli ndani ya mchezo wa soka, Wapenzi hao ni Muhtasham na mkewe, Ihsan.

Mwaka 2015, Muhtasham alionyesha dalili za ugonjwa, lakini bado alihakikisha anahudhuria mechi za Fenerbahçe na Ihsan, ambaye alikuwa na uwezo wa kusimulia kila kitu kinachotokea baada ya mechi.

Mwaka 2016, Ihsan alikaa peke yake kwenye zile siti baada ya Muhtasham kufariki, aliendelea kuhudhuria mechi bila kukosa, licha ya huzuni kubwa aliyokuwa nayo.

Mwaka 2020, Ihsan naye alifariki, Waliacha viti vyao vikiwa tupu, Mashabiki kwa kuheshimu uwepo wao wakaeka picha zao kwenye zile siti walizokuwa wamezoea kuwaona wakiwa pamoja wamekaa.

Ihsan na Muhtasham… hadithi yao ya mapenzi haijafutika mpaka leo katika uwanja wa Fernerbahçe❤️.

💥🇸🇪 Ibrahimovic:"Nilivyokuwa Juventus tulicheza dhidi ya Inter. Materazzi alinichezea rafu mbaya k**a vile muuaji na kun...
22/02/2026

💥🇸🇪 Ibrahimovic:

"Nilivyokuwa Juventus tulicheza dhidi ya Inter. Materazzi alinichezea rafu mbaya k**a vile muuaji na kuniumiza. Miaka minne baadaye, alinijia na nikampiga kwa taekwondo. Nilimpeleka hospitali. Stankovic aliniuliza: ' kwa nini ulifanya hivyo?' Nilimwambia: 'Nimekuwa nikingojea hii nafasi kwa miaka minne.'" 😂🙌

Zlatan kisasi katoka nacho Juventus kaja kulipa kipindi yupo Ac Milan🙌🙌😂😂😂.

Address


Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Vitimbi vya soka posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Vitimbi vya soka:

Shortcuts

  • Want your business to be the top-listed Event/venue?

Share