16/04/2026
STYLE YA UCHEZAJI
Ukifuatilia Post yangu ya mwisho nilisema kiuchezaji Young Africans Sports Club wamebadilika kiuchezaji baada ya ujio wa Amoarim assistant coach mpya
Hawa Mbeya City waliopokea robo tatu wiki ndio hawa hawa waliotoa sare pale mbeya hata wangeongeza dakika 10 kulikuwa hakuna namna ya Yanga kupata bao ile siku lakini leo hata ingeongezwa sekunde ingezaa bao
YANGA WANACHEZA MPIRA WAO SASA
Kutokana na presha kubwa na kasi ya mchezo, Mbeya City walibanwa kucheza ndani ya nusu yao, wakashindwa kujenga mashambulizi yenye tija. Walilazimika kupiga mipira mirefu isiyo na mwelekeo, hali iliyowapa Yanga urahisi wa kurejesha umiliki na kuanzisha mashambulizi mapya
Yanga waliingia uwanjani wakiwa na mpango madhubuti wa kiufundi uliolenga kuudhibiti mchezo mapema kabisa.
Wakitumia mbinu ya high pressing kwa ufanisi mkubwa k**a zamani chini ya Miguel Gamondi na Ramovic Walikuwa wanapandisha presha kuanzia juu kabisa ya uwanja, wakilazimisha wachezaji wa Mbeya City kufanya maamuzi ya haraka chini ya shinikizo kubwa hakuna back pass, Israel mwenda na Mudathuri wamebadilika
Hii ilisababisha makosa mengi ya upotevu wa mipira, hasa katika eneo la ulinzi na kiungo cha chini cha Mbeya City
Baada ya kufanya mabadiliko ya wachezaji, Mbeya City walionekana kuongeza uhai wa mchezo, wakipata nguvu mpya hasa kwenye kasi na mzunguko wa pasi.
Hii iliwapa uwezo wa kusogea mbele kwa ujasiri zaidi na kupunguza presha waliyokuwa wanakabiliana nayo awali
Mbeya City waliingia uwanjani bila tahadhari ya kutosha dhidi ya Yanga, wakionekana wamerelax kupita kiasi. Hali hiyo ilifanya mchezo kuwa wazi zaidi, jambo lililoipa Yanga nafasi kubwa ya kutawala na kuumiliki mchezo kirahisi(wamestahili hiki kipigo)
Mudathili alikuwa k**a rada tu uwanjani ikiichezesha timu atakavyo kiungo wa mpira
Kilichovutia zaidi ni goli la tano la Zimbwe Jr, akimalizia kwa utulivu diagonal pass yenye ubora kutoka kwa Allan Okelloβufanisi mkubwa kwenye final third
Pillar Kelvin ni mali sana akiwa na mpira amekuwa na mchezo mzuri leo
Pacome Zouzoua π₯ π₯ π₯ hakuwahi kuwa na show mbovu "Fantastic player" Allan Okello anajua kucheza anajua kupasi na kuasist pia π₯ what a man, all in all six bila bao fresh tu