01/08/2025
📰 Habari ya Michezo
Liverpool, Uingereza – Klabu ya Liverpool imeanza mazungumzo rasmi na Newcastle United kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Uswidi, Alexander Isak.
Kwa mujibu wa taarifa za , Liverpool tayari wamewasilisha ofa ya awali, lakini Newcastle wameikataa. Hata hivyo, Isak ameeleza wazi dhamira yake ya kutaka kujiunga na The Reds.
Kwa sasa hakuna mazungumzo mapya juu ya mkataba mpya kati ya Isak na Newcastle, huku Liverpool wakipanga kurudi na ofa nyingine hivi karibuni.