11/07/2023
2.Wakati huo hapakuwa na sheria za usalama wa ndege za ndani au za kimataifa nchini Marekani. Unaweza kubeba bomu au bunduki na kwenda moja kwa moja ndani ya ndege.
"Wacuba wanaoishi Marekani walikuwa wanaweza kuteka ndege wakiwa wamewaelekezea bunduki na kutaka ndege iruke kuelekea nchini kwao. Ndege hiyo ikitua Cuba, abiria waliotekwa wanapewa kinywaji kizuri cha gharama Cuba na sigara za Cuba na maafisa wa uwanja wa ndege wa Cuba k**a zawadi, na baadwe wangeruhusiwa kurudi kuendelea na shughuli zao," William alisema. .
Kila kitu kilikuwa cha kufurahisha ... hadi suala la utekaji wa Cooper lilipojitokeza. Kidogo aina ya utekaji wake ilikuwa tofauti. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mtekaji kudai kikombozi katika utekaji nyara huu. Cooper katika safari hiyo alivalia suti nzuri zinazovaliwa sana na wafabiashara akivaa na miwani nyeusi, alionekana mtanashati wakati akipanda ndege.
Alipopanda alimuita mhudumu kwa simu za ndege na kumkabidhi kikaratasi. Muhudumu huyo alidhani mwanaume huyo alikuwa akimtania. Kwa sababu tukio k**a hilo la kupewa barua ama kikaratasi lilikuwa jambo la kawaida sana wakati huo.
Kwa sababu ya matangazo ya mashirika ya ndege ambayo yalikuwa yakufurahisha wateja zaidi kwa mfano tangazoi k**a vile 'Angalia nguo za mhudumu wetu wa ndege', au 'Keti kwenye ndege yetu na ufanye ngono nami (bila shaka, mhudumu ni mzuri').
Kwa mtekaji Cooper nini kiliendelea?
Jina la muhudu aliyepewa kikaratasi alikuwa anaitwa Florence Shatner. Cooper akamkabidhi barua, huku akiendelea kumtazama. Mtu huyu alikuwa tofauti na watu wengine wa kutaniana, pia alikuwa na sura tofauti. Alisema, "Fungua barua hiyo na uisome."
Alikabidhi barua hiyo kwa mhudumu mwingine hewa, Tina McClure. Tina akaifungua, barua hiyo ilisema, "ndege yako imetekwa, nina bomu, njoo uketi karibu yangu."
Tina ilibidi akubali kuketi karibu yake, Cooper akafungua mkoba wake, na kumuonyesha Tina kulikuwa kitu kinachoonekana k**a bomu ndani. Kulikuwa na vijiti vya baruti (kiberiti), kulikuwa