26/01/2024
Wakati Mheshimiwa Rais amefungua fursa za utalii nchini, eneo mojawapo lenye fursa kubwa ya kuchangamkia ni kuku wa asili.
Kuku wetu wa asili anautangaza utamaduni wa Kitanzania. Kila mgeni anayeingia nchini, bila shaka kuku wa asili atakuwa ni moja ya kitoweo cha kumkaribisha.
Ladha nzuri ya kuku wetu wa asili na ubora wake, ni kitu pekee kinachoweza kufungua na kukuza masoko ya kuku wa asili kimataifa.
Ndio maana tunapomzungumzia kuku wa Horasi, tayari tunamuweka kuku huyu kwenye sura ya kushindana na soko la Kimataifa na kuingiza fedha nyingi kwa nchi yetu.
Wakati inaonesha ifikapo 2030 tutakuwa na uhaba mkubwa wa nyama ya ng'ombe na mbuzi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa yanayoathiri malisho, sehemu pekee itakayotegemewa kwa sana kutoa nyama ni kwenye sekta ya kuku.
Hii inatuonesha kwamba inatakiwa tujiandae, na kuandaa vijana waione fursa na kuanza kuchangamkia mapema.
Ndio sababu kubwa ya miongoni mwa malengo yake kwa wanafunzi ni kutoa fursa ya mafunzo ya stadi za maisha na ujasiriamali katika tasnia ya kuku wa asili ili kuhakikisha wanafunzi wanaanza kujiandaa mapema katika ushindani huo.
Sababu kubwa ya kuku wa asili mbali na kutangaza utamaduni wa kitanzania, ila kuku huyu anafugika kwa gharama ndogo sana na ana uwezo wa kuzaliana. Hivyo anatoa fursa kwa vijana au wanafunzi kutumia muda wa ziada katika kufuga ili kujiongezea kipato na kukabiliana na changamoto za lishe duni na ajira.
Kuku wa asili anafugika vizuri kibiashara, na anakua kwa wakati endapo tu utakuwa na mbegu bora na elimu ya kutosha katika ufugaji.
.
Milango ya udhamini imefunguliwa tayari, kuwasiliana nasi piga simu 0769409240/0758061582.
m
tz