05/06/2026
🚨 WHY TV ZA NCHI ZINAONESHA MECHI CHACHE ZA KOMBE LA DUNIA!?
Kumekuwa na maneno mengi kuwa “TV za Taifa zinaonesha mechi chache au wanachagua kuonesha mechi za michuano fulani”
SIO KWELI…!
Wao hawajichagulii mechi za kuonesha. FIFA kupitia wateja wao wa kwanza wanaowauzia haki za matangazo wanaweka ukomo wa mechi za kuoneshwa na TV za Taifa (Public Broadcasters) na wao huwaweka kwenye kundi la FTA (Free to Air).
Wanafanya hivyo ili kulinda Biashara ya matangazo kwa sababu chaneli hizo za Taifa zote ni Bure duniani. Hivyo hakuna mtu atakayekuwa tayari kulipia kitu ambacho anaweza kuona bure hata angekuwa kichaa.
Mfano…! Kusini mwa jangwa la Sahara Idhaa zote za Taifa zimepewa mechi 34 tu na wao wanahakikisha walau mechi 1 au 2 kwa siku.
Kikubwa hawatakunyima Mechi za muhimu kwenye hatua muhimu. Mfano! Fainali, Mshindi wa Tatu, Nusu n.k.
Hivyo basi…! Channel zote za Taifa hakuna inayojiamulia mechi…! Na haziuziwi mechi zote hata ungepeleka pesa gani…!
Unapangiwa mechi kulingana na ukanda wako…! Kuna Senegal vs England na kuna Croatia vs Ujerumani!? Watakuzingatia kwanza kwa Senegal kulingana na ‘proximity’ yenu ambayo ni Geographical au Psychological.
VIPI KUHUSU MUONEKANO!?
Hili sio suala lao pia.
Kwa kawaida wauzaji wa matangazo wanatoa LINK ambayo wote mnaipata moja ndio maana ikikata kwa mrusha matangazo mmoja lazima wote mpotee hewani kwa ukanda huo.
Suala la ubora wa picha linategemeana na mambo mawili makubwa…! Picha yenu mnayopokea mnaitoaje au wamiliki wa ving’amuzi vya hiyo Televisheni wataminya au kufifiisha picha kwa kiwango gani.
Wapo wanaobana Ubora kwa sababu za kibiashara na ushindani au vinginevyo hivyo unakuta channel inaachia 1080 au 4K ila wao wanaminya pahali…!
Ndio maana chaneli hiyo moja moja unakuta inaonesha mpira kwa ubora tofauti kulingana na king’amuzi husika✍️
Tarajia hivyo kwa TBC, UBC, SABC, KBC na chaneli zote za Taifa.
Ameandika ✍️
nazareth_upete