26/06/2023
CANNAVARO WAFUNGULIE DARASA LA MAHOJIANO WAZENJI WENZAKO.
Na
Yassin Jiwe
Moja kauli ambazo kaka yangu hupenda kuzitamka tukipiga story ni kwamba "usizungumze vitu hasi vya mwajiri wako wa zamani katika ajira Yako mpya". Moja kitu kinachofanyiwa kazi na hao waajiri wapya ni kupima uwezo wako wa kuhimili changamoto mahala pa kazi na utendaji wako.
Zanzibar k**a kisiwa kina Sifa nyingi sana katika tasnia tofauti iwe Muziki utawakuta habari za Bibi Kidude na wengine. Iwe michezo pia.
Klabu ya Yanga imekuwa na bahati ya kupata vipaji vya kutoka Zanzibar na kuichezea klabu Yao kwa kiwango kuzuri mno. Achana na kazi chafu za Ibra Bacca,Shaibu Ninja. Umahiri wa Mudathir Yahya Abbas unao uona.
Wamepita Wazanzibar Wengi katika ubora wao iwe walinda mlango k**a Riffat Hamis na hata Walinzi ,viungo na Washambuliaji pia. Binafsi sijawahi kuona kipaji Cha Kizanzibar kilichokuja Yanga au Simba kisifanye kazi iliyomleta. Hata Ally Ahmed Shiboli ana jina lake pale Simba.
Unamfahamu Nadir Haroub Ally 'Cannavaro' 'Upapa'. Ndiyo nataka kusema kuhusu yeye na Sio Abdi Kassim Baby' 'Ballack wa unguja'. Usishtuke kwa haya majina ya Ballack Wala Cannavaro ni kawaida ya Wazanzibar Wengi kutumia majina kupachikwa na jamaa zao au kujipachika wao. Happy ndo unawakuta kina Bacca, Ninja ,Shiboli, Ballack, Cannavaro, Feitoto,Bui,Makapu na wengine wengi.
Twende na Cannavaro, katika orodha ya watu kutoka Zanzibar wameweka alama ya muhuri wa moto katika klabu ya Yanga Toka Zanzibar basi ni Nadir Haroub Ally 'Cannavaro''Upapa'. Hakuna mtanzania asiyeijua kazi yake. Hakuna mtanzania ambaye alitia shaka akimwona katika jezi ya Yanga au timu ya Taifa. Upapa alikuwa mwamba alikuwa bedui alikuwa katili katika nyasi za uwanja wa mchezo wa soka. Lakini akiziacha zile Nyasi ni mtu mmoja poa sana ana hekima ana busara haoengei ongei pasipo na sababu na mtulivu wa kusikiliza pia.
Nilicheka sana baada ya kuisikiliza interview ya Mbwana Samatta baada tu ya kusajiliwa na Aston villa. Niligundua Mbwana alipangwa na alijua natakiwa kuongea nini baada ya kupitishwa kwenye maswali. Samatta ni Shabiki wa haswa wa Manchester united FC na kidogo Real Madrid sababu ya Karim Benzema na hata mwanae wa kiume anaitwa Benzema (Karim). Ila alimwelezea Gabriel Agbonlahor mshambuaji wa zamani wa Aston villa utadhani kweli alikuwa akimfuatilia sana. Agbonlahor ndiye mshambuaji anayeongoza rekodi ya kufunga magoli mengi kwa muda wote pale Aston villa. Ilikuwa lazima Mbwana ajue anaenda kucheza alipocheza Agbonlahor ila hapa alipangwa. Akawataja kina Emily Heaskey na wengine .Aliandaliwa katika muktadha chanya.
Naikumbuka mechi moja ya Yanga ya Ligi kuu Cannavaro alitofautiana na Juma Abdul wakarushiana maneno alitimiza jukumu lake k**a kiongozi kwa mchezaji wake lakini Juma hakupokea kwa kukubali. Jambo lililofanya Hadi wanaenda mapumziko wachezaji wenzao wawashike wasiweze kupigana. Hapa unawazungumzia Wachezaji ambao walikuwa kuwa manahodha wa Klabu. Tafsiri ya wazi ni uchungu kutokukubali kushindwa Ari ya kupambana ndiyo iliyozua hiyo tafrani.
Asilimia kubwa ya wachezaji walioanza kuonekana katika luninga kwenye Ligi kuu hasa wale manahodha walikopi utulivu,umakini na upangiliaji wa maneno wanapofanya mahojiano na waandishi baada ya mchezo kutoka Nadir Haroub Ally 'Cannavaro''Upapa'. Huyu ndo wakati Ligi kuu inaanza kuoneshwa ilikuwa mwandishi anafurahia utiririkaji wa maneno na mpangilio wa hoja unaotolewa na Nahodha baada ya mchezo. Huyu ndiye Aliyekuwa na kawaida ya kuanza na "Namshukuru mwenyezi Mungu kwa matokeo,pia nawashukuru wachezaji wenzangu kwa mchango wao katika timu na nawapongeza wapinzani wetu ni wazuri wametupa changamoto kubwa wana timu nzuri". Aina hii ya maneno Toka kwa manahodha iliasisiwa na Cannavaro,unawaheshimu wapinzani na kuwapa credit Yao.
Hapo awali manahodha na makocha wengi waliongea ovyo sana mbele ya media yakawa maneno k**a " tulijua tutawafunga ila hatukujua tu ni idadi Gani, hawa wakawaida sana hawana maajabu" na maneno mengine ya kukosa kuheshimu like kinachofanywa na wenzenu. Hii ilikuwa kwa makocha na Wachezaji pia.
Kuna mchambuzi mmoja nguli legend katika kazi hiyo ni rafiki mkubwa wa Cannavaro tangu walipokutana katika siku ya kwanza alipoitwa timu ya Taifa na Marcio Maximo na wakasafiri Hadi Msumbiji katika mechi ya kufudhu Afcon.
Mchambuzi huyo alipoufahamu utulivu na umiaji sahihi wa maneno mbele media alipomhoji Cannavaro akagundua jamaa ni Smart kichwani. Akawa karibu naye na kufundisha upangiliaji wa mawazo na uteuzi wa maneno ya kuongea mbele ya media.
Cannavaro akawa anapewa baadhi ya clip za manahodha wa b
Vilabu vikubwa ulaya wanavyo zungumza na Media kabla na baada ya mechi. Hali Ile ikawa inamjenga na kujua namna ya kukitumia kinywa na ulimi wake vizuri. Hii ilimfanya jamaa ajiamini kuongea mbele ya media yoyote iwe ya lugha ya Kiingereza au Kiswahili.
Moja mahojiano mazuri yaliyonifurahisha binafsi Cannavaro alihojiwa na mwandishi wa Super sport katika moja ya mechi ya Taifa Stars. Kwa namna ambavyo Cannavaro alishusha Kiingereza katika kuelezea mchezo ilitosha kusema huyu hakika ni Nahodha. Hivi si umesikia yule Mwalimu wa Diamond kwasasa anamfundisha Bakari Nondo Mwamnyeto?.
Iliwahi kutokea katika mechi ya Burkina Faso dhidi ya Tanzania pale Ouagadougou.Mechi iliyomalizika kwa Ushindi kwa Tanzania goli la Erasto Nyoni. Baada ya filimbi ya Mwamuzi ,media zilimfuata Nahodha msaidizi Salumu Swedi Aliyekuwa kavaa usinga baada Nahodha mkuu Shadrack Nsajigwa Mwandemele kupata kadi nyekundu pamoja na kocha Marcio Maximo.Salum Swed alichokifanya akamvuta Danny Mrwanda ili aongee na Wale waandishi wa habari.Unajua kwanini? Jibu unalo.
Cannavaro inasemekana alikuwa akitazama sana mahojiano ya John Terry Nahodha wa Chelsea na England wakati huo lakini pia alimfuatilia sana mahojiano ya Manahodha wengine wa vilabu vya ulaya. Hii ilimjenga na kumfanya kuwa yeye na wengine wakawa wanaiga kwa Cannavaro.
Utulivu umakini uteuzi wa maneno mpangilio wa mawazo katika kuzungumza ndicho kitu pekee ambacho kinaweza kupima uwezo wa akili wa Kila mtu.
Mtu unaweza kuwa na hoja ya Msingi lakini ukishindwa kuipangilia na kuipa uteuzi mzuri wa maneno ya kuongea sambamba na kupangilia mawazo yawe katika mtiririko wenye kuleta maana kwa msikilizaji utaonekana k**a unapiga kelele na sio kuwasilisha hoja.
Watu ambao wanafuatiliwa kwa karibu na jamii iwe kisiasa kiuchumi kiutamaduni iwe kimichezo lazima ujifunze namna ya kuwa na uteuzi wa maneno , upangiliaji wa hoja na mtiririko wa mawazo yenye kuleta maana ya unacho kizungumza maana kitawafikia wengi. Hili hujifunzi siku moja ni jambo la Kila wakati unajifunza ili kuwa Bora zaidi na zaidi. Hiyo ndo sisi tuliosoma Chad tunaiita PR na tunaitumia sana.
Mara kadhaa nilikuwa najiuliza kwanini Yanga walimteua kipenzi changu katika soka eneo la Kiungo Feisal Salumu Abdallah kuwa Nahodha. Nilijiuliza baada ya kujiridhisha kuwa hajui kufanya mahojiano kabla ya mchezo na baada ya mchezo. Utulivu umakini uteuzi wa maneno ya kuongea ni kitu kilichokuwa bado sana kwake. Yaani Media ilikuwa haipati kitu walicho kitamani Toka katika kinywa Cha Feitoto ambacho ninatokana na miguu yake au kazi ya timu kwa ujumla.
Ina maana Cannavaro hakuwafundisha Wazenji wenzake namna ya kuzungumza na Media unatakiwa kufanya nini. Ina maana hata hawawatazami wachezaji wengine.
Hata Ronaldo alipofanya Mahojiano yake ya mwisho akiwa Uingereza kabla ya kombe la Dunia ,walao ilikuwa na uzito wake. Lakini si hii ya Mwanangu Fei na power breakfast ya Clouds fm. Huwezi ifananisha na Ronaldo sababu maudhui ya Ronaldo alilaumu kwa kuibua changamoto na kukosoa mfumo na alitoa ufanano wenye mwelekeo chanya kwa klabu akilinganisha uzoefu wake aliopata kwa vilabu vingine. Ila Sasa Kuna mwanetu wa Fuoni huyo ni kanyaga twende mtajijua wenyewe. Hii ndo tafsiri ya makuzi yetu na kiwango chetu Cha akili katika matumizi yake ambacho kinasababishwa na ukosefu wa maarifa ambayo Mungu hataki kuona tukiangamia kwa kukosa maarifa.