Halisi Max

Halisi Max Updates 24 Hrs

Takriban waendesha pikipiki 100 walikusanyika nje ya Msikiti wa Kaunas nchini Lithuania wakati Waislamu wakiendelea na S...
14/09/2026

Takriban waendesha pikipiki 100 walikusanyika nje ya Msikiti wa Kaunas nchini Lithuania wakati Waislamu wakiendelea na Swala ya Ijumaa.

Waendesha pikipiki hao walivurumisha injini, kupiga muziki kwa sauti kubwa, kupiga kelele na kuwarekodi waumini waliokuwa katika ibada.

Inadaiwa pia kuwa kundi hilo lilifika na kichwa cha nguruwe na kuwaonyesha waumini waliokuwa wakiendelea na ibada katika eneo la msikiti, jambo ambalo jamii ya Waislamu imelielezea k**a kitendo cha makusudi cha kuwatisha na kuwafedhehesha waumini wakati wa ibada.

Pamoja na usumbufu huo, waumini walibaki watulivu na waliendelea na Swala yao hadi mwisho.

Polisi nchini Lithuania wameanzisha uchunguzi wa kiutawala ili kubaini iwapo tukio hilo linaweza kuhusisha uchochezi au vitendo vinavyolenga kundi fulani la watu.

Jamii ya Waislamu ya Kaunas imelaani tukio hilo na kusisitiza kuwa uhuru wa dini unapaswa kumruhusu kila mtu kuabudu kwa amani, usalama na bila vitisho.

Una maoni gani kuhusu tukio hili?

Kauli ya Asnat Cute imeibua mjadala kuhusu ukubwa wa matiti na namna jamii inavyohusisha mwonekano wa mwanamke na mambo ...
14/09/2026

Kauli ya Asnat Cute imeibua mjadala kuhusu ukubwa wa matiti na namna jamii inavyohusisha mwonekano wa mwanamke na mambo k**a kunyonyesha au matumizi ya ngono.

Asnat amesema ana miaka 22 na mtoto mmoja ambaye ndiye pekee aliyemnyonyesha, lakini licha ya kuwa anaoneka ana matiti makubwa haelewi yatakuwa yamefika wapi atakapotimiza miaka 30.

Amesisitiza kuwa hali hiyo si kwa sababu ameyatumia sana k**a baadhi ya watu wanavyodai, bali anaamini ni maumbile yake.

"Jamani Mimi Nina miaka 22 Nina Mtoto mmoja tu niliyemnyonyesha licha ya Kuwa Nina maziwa makubwa Ziwa langu ni ndala lakini Mtoto wangu ni Mmoja tu, swala la Ziwa langu Kuwa ndala wengi mnasema nimelitumia sana sio kweli sijalitumia sana ndio kwanza Nina miaka 22 sema tu nimaumbile jamani Mimi mwenyewe Huwa Najiuliza k**a nyie mnavyojiuliza nikitimiza miaka 30 yatakuwepo wapi" Amesema Asnat Cute

Kwa upande mwingine, mjadala huu unaonyesha jinsi ambavyo watu wanavyokuwa wepesi kutoa hitimisho kuhusu miili ya wengine bila kujua historia au sababu halisi ya mwonekano wao.

Wewe unaonaje kauli ya Asnat? Ni maumbile tu au kuna mambo mengine yanaweza kuchangia ukubwa wa matiti? ๐Ÿ‘€๐Ÿ‘‡

Mwanasiasa Godbless Lema ameeleza sababu ya kuchapisha ujumbe wa kutoa pole kwa Rais Samia Suluhu Hassan, huku akimnukuu...
14/09/2026

Mwanasiasa Godbless Lema ameeleza sababu ya kuchapisha ujumbe wa kutoa pole kwa Rais Samia Suluhu Hassan, huku akimnukuu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, ambaye alitoa salamu za pole akimuagiza Makamu wake Heche Azifikishe kwa Rais Samia kufuatia kufiwa na Mume wake Marehemu Maalim Hafidh Ameir.

Lema amesema ameshuhudia matusi na sintofahamu nyingi mtandaoni kufuatia ujumbe huo, akisisitiza kuwa kwa jamii inayodai kupigania uhuru wa maoni na demokrasia, kutofautiana kwa hoja hakupaswi kuwa sababu ya matusi, dhihaka wala chuki.

Kwa mujibu wa Lema, Lissu ambaye amekaa gerezani kwa takribani mwaka mmoja na miezi sita akikabiliwa na kesi ambayo wao wanaamini ni ya kisiasa na isiyo na haki, bado aliweza kutoa salamu za pole baada ya kufahamishwa kuhusu msiba wa mume wa Rais Samia.

Lema amesema Lissu alitoa salamu hizo za pole mara mbili akiwa mbele ya mahak**a, jambo ambalo amesema si unyonge, bali ni hekima, utu na ukomavu wa kiwango cha juu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika โœ๏ธ
โ€”โ€”
Nimeona matusi na sintofahamu nyingi mtandaoni baada ya kuchapisha ujumbe wa kutoa pole kwa Mama Samia, hasa niliponukuu salamu za pole za Mwenyekiti Lissu kutoka gerezani.
Kwa sisi jamii tunaodai kupigania uhuru wa maoni na demokrasia, hili linapaswa kutufikirisha. Kutofautiana kwa hoja hakuhitaji matusi, dhihaka wala chuki.

Lissu amekaa gerezani takribani mwaka mmoja na miezi sita, akikabiliwa na kesi ambayo sisi tunaamini ni ya kisiasa na isiyo na haki. Anafahamu yaliyompata na serikali iliyomweka mahabusu. Lakini alipofahamishwa kuhusu msiba wa mume wa Mama Samia, akiwa mbele ya mahak**a, alitoa salamu zake za pole kwa wafiwa mara mbili.

Huu si unyonge. Hii ni hekima, utu na ukomavu wa kiwango cha juu.
Na si mara ya kwanza. Aliwahi pia kumtetea Sabaya katika kesi yake Moshi. Wengi tulishangaa, nami nilishangaa. Lakini nilipomuuliza baadaye, nilielewa kwamba kwake haki haichagui upande.

Mchambuzi wa michezo kutoka Azam Sports, Michael Hyera, ameuaga rasmi ukapera baada ya kumuoa mpenzi wake Winnie, na sas...
14/09/2026

Mchambuzi wa michezo kutoka Azam Sports, Michael Hyera, ameuaga rasmi ukapera baada ya kumuoa mpenzi wake Winnie, na sasa wanaanza safari mpya ya maisha k**a mke na mume. โค๏ธ๐Ÿ’

Jana tulishuhudia mchezaji wa Azam FC, Yahaya Zayd, akifunga ndoa na mtangazaji wa Azam Media, Fatma Chikawe. Leo tena tunasikia habari ya ndoa ya Michael Hyera na Winnie.

Kwa namna hii, Azam TV inaonekana k**a imeamua mwaka huu uwe wa ndoa! ๐Ÿ˜‚
Kinachovutia zaidi ni kwamba watu wa Azam wanaonekana kuishi msemo wa โ€œukifanya kazi sehemu moja, unaweza pia kupata mwenza wako hapo hapo.โ€ ๐Ÿ˜…

Hongereni Michael Hyera na Winnie. Mungu awajalie ndoa yenye upendo, amani na baraka. ๐Ÿ™

Esma Platnumz, dada wa Diamond Platnumz, amezungumzia tabia ambayo amesema haipendezi kutoka kwa wifi yake Zuchu.Kwa muj...
14/09/2026

Esma Platnumz, dada wa Diamond Platnumz, amezungumzia tabia ambayo amesema haipendezi kutoka kwa wifi yake Zuchu.

Kwa mujibu wa Esma, pale Zuchu anapokosana na Diamond, amekuwa na tabia ya kuwazuia (block) watu mbalimbali wa familia, akiwemo wifi yake, mkwe wake, mashemeji na hata baadhi ya wafanyakazi wa Wasafi.

Esma amemtaka Zuchu kuacha tabia hiyo na kusema kwa sasa akiwa mama anapaswa kuwa mtu wa kutulia zaidi na kuacha mambo ya utoto.

Lakini hapa ndipo swali linapoanziaโ€ฆ ๐Ÿค”
Je, Zuchu kweli ana tatizo la kutokuwa na uvumilivu au hii ni namna yake ya kuweka mipaka anapokuwa amekasirika?

Kwa sababu ukweli ni kwamba, tabia ya mtu kublock watu kila anapokasirika inaweza kuonekana k**a njia ya kujilinda na kuepuka mawasiliano wakati wa hasira.

Lakini upande mwingine, k**a kila kutofautiana kunapelekea familia nzima kuingia kwenye block list, hapo inaweza kuleta picha kwamba migogoro ya watu wawili inageuka kuwa mgogoro wa familia nzima.

Na hili la Zuchu kuwablock watu kwenye Instagram pia si jambo geni kusikika. Kuna watu mbalimbali ambao wamewahi kulalamika kuhusu kuzuiwa na msanii huyo.

Lakini pia tusisahau, kuwa Superstar hakumaanishi mtu hana hisia au hawezi kukasirika. Umaarufu unahitaji moyo mgumu, lakini pia kila mtu ana namna yake ya kushughulikia hasira na migogoro.

Swali kubwa ni hili ๐Ÿ‘‡
Zuchu anatakiwa kuacha kabisa tabia ya kublock watu anapokasirika, au kila mtu ana haki ya kumzuia mtu asiyemtaka kwenye maisha yake?
NENO LAKO HAPA ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ

Wakati mwingine thamani ya mtu maarufu haipimwi kwa ukubwa wa jina lake, bali kwa namna anavyotumia nafasi aliyonayo kuw...
14/09/2026

Wakati mwingine thamani ya mtu maarufu haipimwi kwa ukubwa wa jina lake, bali kwa namna anavyotumia nafasi aliyonayo kuwagusa watu wenye uhitaji.

Najath Ibrahim, binti mwenye umri wa miaka 20 na mwanafunzi wa CBE, amepitia changamoto kubwa baada ya figo zake zote mbili kushindwa kufanya kazi.

Kwa sasa anahitaji takribani TSh milioni 40 kwa ajili ya matibabu, huku kila wiki akihitaji karibu TSh 600,000 kwa ajili ya Dialysis.

Lakini muda mfupi baada ya video ya Najath kusambaa akiomba msaada, Niffer amejitokeza na kuchangia TSh milioni 2 baada ya kuiona video hiyo.

Milioni 2 inaweza isiwe mwisho wa safari ya Najath, lakini inaweza kuwa mwanzo muhimu sana wa safari yake ya kuokoa maisha.

Jambo jingine kubwa zaidi ni kwamba, pamoja na matibabu, Najath anahitaji pia mfadhili anayefaa kwa ajili ya kumpa figo moja, jambo ambalo linahitaji utaratibu na tathmini za kitabibu.
Hongera Niffer. ๐Ÿ™

Katika dunia ambayo watu wengi huonekana kupitia umaarufu wao, wewe umeonyesha kwamba umaarufu unaweza pia kuwa daraja la kumsaidia mtu mwingine kuendelea kuishi.

Sasa swali ni moja: Je, tutashirikiana kumsaidia Najath kufikisha hiyo milioni 40?
Kila mchango una maana. โค๏ธ๐Ÿ™

14/09/2026

JE, NI KWELI MWENZA WAKO MARA NYINGI UNAMPATA KWENYE CIRCLE YAKO? ๐Ÿค”๐Ÿ’

Kuna msemo unaosema, โ€œAsilimia kubwa ya watu wanaooana hukutana kupitia circle zao.โ€ Maana yake ni kwamba mazingira unayoishi, kufanya kazi au kujihusisha nayo yanaweza kuongeza nafasi ya kukutana na mtu mwenye muelekeo unaofanana na wako.

Ukiwa mfanyabiashara, mara nyingi unaweza kukutana na mwenza kupitia biashara. Ukiwa askari, unaweza kukutana na mtu kupitia mazingira ya kazi yako. Ukiwa kwenye burudani, unaweza pia kupata mwenza kwenye mazingira hayo.

Mfano wa sasa ni Yahaya Zayd na Fatma Chikawe. Wawili hawa wamekutana kupitia mazingira ya Azam, mmoja akiwa mchezaji wa Azam FC na mwingine akiwa mtangazaji wa Azam TV, na leo wamefunga ndoa. โค๏ธ๐Ÿ’

Hii inatufanya tujiulize: Je, mazingira tunayochagua kuwa sehemu ya maisha yetu yana mchango mkubwa katika kumpata mwenza wa maisha?
Au ni kwamba mapenzi hayana formulaโ€”unaweza kukutana na mtu wako mahali popote, bila kujali circle yako?

Hongereni Yahaya Zayd na Fatma Chikawe kwa hatua hii kubwa ya maisha. Mungu awajaalie ndoa yenye upendo, amani, kheri na baraka. ๐Ÿคฒโค๏ธ

WEWE UNAAMINI MWENZA WA MAISHA MARA NYINGI ANAPATIKANA KWENYE CIRCLE YAKO? ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amewasili Mkoani Tabora kwa ziara ya siku nne, ambapo atatembe...
14/09/2026

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amewasili Mkoani Tabora kwa ziara ya siku nne, ambapo atatembelea Halmashauri za Sikonge na Uyui kukagua na kutathmini utekelezaji wa miradi ya afya inayosimamiwa na Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF).

Katika ziara hiyo, Dkt. Kikwete anatarajiwa kutembelea zahanati zilizojengwa kupitia taasisi hiyo pamoja na kufuatilia utekelezaji wa Mradi wa Jamii Salama, unaolenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya ya mama na mtoto kwa urahisi zaidi.

Mbali na kukagua miradi hiyo, ziara hiyo itatoa fursa ya kupata mrejesho kutoka kwa wananchi kuhusu namna miradi hiyo inavyotekelezwa na mchango wake katika kuboresha huduma za afya, hususan kwa akina mama na watoto.

Urembo ni kitu ambacho mara nyingi hutofautiana kulingana na macho ya mtu, lakini safari hii jina la Lingling Kwong lime...
14/09/2026

Urembo ni kitu ambacho mara nyingi hutofautiana kulingana na macho ya mtu, lakini safari hii jina la Lingling Kwong limeibua mjadala mkubwa.

Mwigizaji na mwanamitindo huyo mwenye miaka 31 kutoka Thailand ametangazwa kuwa Most Beautiful Woman Alive 2026 baada ya kupata zaidi ya kura milioni 22, akimpiku mshindi wa mwaka 2025, Sila Turkoglu wa Uturuki.

Kitu kinachovutia hapa si tu jina la Lingling, bali idadi kubwa ya kura alizopata. Kura milioni 22 zinaonyesha ukubwa wa ushawishi na nguvu ya mashabiki alionao, hasa katika kizazi hiki ambacho mitandao ya kijamii imekuwa sehemu kubwa ya mashindano k**a haya.

Lakini pia kuna swali la kujiuliza: Je, kura nyingi zinamaanisha mtu ndiye mrembo zaidi, au zinaonyesha zaidi ukubwa wa mashabiki wake? ๐Ÿ‘€
Kwa sababu uzuri hauna kipimo kimoja.

Mtu anaweza kuwa na mashabiki wengi na kupata kura nyingi, lakini mwingine akaonekana kuwa mrembo zaidi kwa mtazamo wa watu wengine.

Wewe umepewa nafasi ya kupiga kura, Lingling Kwong angekuwa chaguo lako? ๐Ÿ˜๐Ÿ”ฅ

Kupitia ukurasa wake wa TikTok, Najath ameandika ujumbe huo wa kugusa moyo huku akiendelea kupambana na changamoto kubwa...
14/09/2026

Kupitia ukurasa wake wa TikTok, Najath ameandika ujumbe huo wa kugusa moyo huku akiendelea kupambana na changamoto kubwa ya kiafya.
Najath ni binti mwenye umri wa miaka 20, ambaye amelazimika kusitisha masomo yake ya chuo kutokana na maradhi aliyoyapata. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, figo zake zote mbili zimefeli na kwa sasa anahitaji matibabu yanayohitaji kiasi cha takribani Shilingi Milioni 40.

Hii ni safari ambayo Najath hawezi kuimaliza peke yake. Ndoto zake bado zipo, na ujumbe wake unaonesha kuwa licha ya hali anayopitia, bado anaamini ipo siku atarudi kwenye maisha yake ya kawaida na kutimiza ndoto zake. โค๏ธ๐Ÿ™

Namba ya Najath 0795013416 โ€” Najati Nurudini Ibrahimu, imezuiwa kwa muda wa saa 24 kupokea miamala baada ya kupokea kiasi cha takribani Shilingi Milioni 4 ndani ya muda mfupi.
Hivyo, kwa sasa michango yote itumwe kupitia Lipa Namba ifuatayo, huku juhudi zikiendelea kutafuta suluhisho la kurejesha uwezo wa namba yake kupokea miamala.

๐Ÿ’ณ LIPA NAMBA: 15868502
๐Ÿ“ฑ MIX BY YAS
๐Ÿ‘ค JINA: MWANACHUO FAMILY
Kiasi chochote unachoweza kutoa kinaweza kuwa sehemu ya safari ya kumsaidia Najath kupata matibabu anayohitaji.

Najath ana ndoto. Najath ana matumaini. Na leo anahitaji sisi kuwa sehemu ya matumaini hayo. ๐Ÿคโค๏ธ
Tumuombee na tumsaidie kwa kile tunachoweza. ๐Ÿ™

Address

Mbezi
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Halisi Max posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share