24/04/2026
KLABU YA SIMBA SC IMEWEKA HISTORY NYINGINE WHATSAPP HUKU REAL MADRID AKIWA NDIO NAMBA MOJA KWENYE ORODHA YA VILABU BORA DUNIANI.
SIMBA YAKIMBIZA DUNIANI.
Kampuni ya utafiti wa masuala ya michezo kidijitali kutoka Ujerumani, RESUILTSsports, imetoa ripoti mpya inayoorodhesha vilabu 20 vya soka duniani vyenye ufuatiliwaji mkubwa zaidi kwenye majukwaa ya WhatsApp Channels. Utafiti huo unaonyesha namna vilabu vikubwa vinavyozidi kutumia majukwaa ya mawasiliano ya moja kwa moja kuwafikia mashabiki wao duniani.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, vilabu vikongwe barani Ulaya vinaongoza orodha hiyo kutokana na ukubwa wa mashabiki wao kimataifa pamoja na uwekezaji mkubwa katika maudhui ya kidijitali. Hata hivyo, jambo la kuvutia zaidi ni uwepo wa vilabu vitatu kutoka Afrika vilivyofanikiwa kuingia kwenye orodha hiyo ya dunia.
Vilabu hivyo ni Kaizer Chiefs kutoka Afrika Kusini, Al Ahly SC ya Misri, pamoja na Simba SC ya Tanzania. Mafanikio haya yanaashiria ukuaji mkubwa wa soka la Afrika kwenye anga ya kidijitali, huku mashabiki wakizidi kuhamia kwenye majukwaa ya kisasa k**a WhatsApp Channels kufuatilia habari, matokeo na taarifa za vilabu vyao.
Ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa matumizi ya WhatsApp k**a chombo cha mawasiliano kati ya vilabu na mashabiki yameongezeka kwa kasi, yakitoa fursa mpya za kibiashara, matangazo na uhusiano wa karibu zaidi kati ya pande hizo mbili.
Kwa ujumla, matokeo haya yanaweka wazi kuwa mapinduzi ya kidijitali yanaendelea kubadilisha namna soka linavyoendeshwa na kufuatiliwa duniani, huku Afrika nayo ikiendelea kujipenyeza kwenye ramani ya kimataifa.
KWA HABARI ZA MICHEZO FOLLOW UKRASA WETU Simonaytz