07/07/2021
⚽️FOOTBALL BUILDUP:...........................................
The Playmaker:
-Ni yule mchezaji ambaye ana control mchezo mzima kwa timu husika offensively playing. Mara nyingi anahusika katika kusambaza mipira kila eneo la uwanja kwa mijongeo ya pass zake zinazopelekea kutengeneza nafasi za magoli.
Playmaker anaibeba timu kupitia vision, ufundi/ ujuzi, ball control yake, ubunifu (creativity), passing ability, maamuzi sahihi (decisive).
Ipi position ya Playmaker?, mara nyingi tumeona kwamba wale centre midfielders ndio huwa wanakuwa playmakers kwenye timu zao maana wao ndio huchukua game.
Hapa kuna attacking midfielders ,wao hucheza zaidi kwenye upper zone wanakaa katikati ya viungo (CM) na washambuliaji (forwards) wanakuwa free role, hujulikana k**a advanced playmaker (Trequartista kwa lugha ya kiitaliano) wanacheza kwenye position ya no.10.
Aina hii ya play maker anaweza kusit katikati ya dimba au akatokea pembeni. Huyu anaichezesha timu akitokea eneo hilo kwa kupiga pass sahihi kuwafikia washambuliaji ama pembeni kwa mawinga,atapiga cross,atatengeneza nafasi za magoli (assists, key passes) na kufunga magoli, atahold Possession on Opponents half kwenye ⅓ ya mwisho ya uwanja.
Playmakers hawa ni highly technical skills, na very tactical intelligence, wapo chapu na wanajua kutembea na mpira, ni wenye vision ya hali ya juu na wana uwezo mzuri wa kushuti, kupiga crosses, kuassist, kupass, kudribble, kufunga na kuanzisha mashambulizi, kutengeneza nafasi za magoli, playmakers wengi wa aina hii ni wazuri kwenye mipira iliyokufa (set pieces) penalt, free kicks, corner, kiufupi ni dead ball specialist. Playmakers hawa mara nyingi wanafiti kwenye mfumo wa 433, 343. Lionel Messi, Eden Hazard, Maradona, Dinho, KDB, ni mfano wa advanced playmakers.
Kuna aina nyingine hii ya playmaker "Deep lying playmaker" huitwa Rejesta kiitaliano. Hawa jukumu lao kuu ni kuchezesha timu kuanzia dimba chini (deep position), wanacheza nyuma kidogo ya mstari wa viungo wa kati na wanaonekana kuwa ni defensive midfielders (holding defensive midfielder) kwani hucheza juu kidogo ya mstari wa ulinzi (defensive line), wanatumia eneo hilo lenye space kuichezea timu nzima kwa pasi ndefu na fupi, hawa hawashambulii kwenda langoni wao wanaituliza timu na kukeep possession from the deep possession. Huwezi kuwaona wakiassist sana ama kufunga.
Deep lying playmaker ni technical, visionable, na wana uwezo mkubwa wa kupiga pass. Wanafahamika zaidi kutokana na uwezo wao wa kupiga pasi ndefu zenye kuvuka mstari wa viungo na mabeki kwenda kwenye forward line. Playmaker wa aina hii pia ni wazuri kwenye tackles na Interceptions. Wanacheza kwenye position ya no.6/8. Aina hii ya playmakers wanafaa kwenye mfumo wa 4231,3421,4141,4123. Andrea Pirlo na Jorginho ni mfano wa deep lying playmaker,
Playmaker sio lazima atokee eneo la midfielder, play maker anaweza kutokea eneo la pembeni akicheza k**a winga, pia anaweza kuwa CF. Kinacho define uplaymaker ni technical ability, good ball control, holding possession (umiliki), game balacing, dribbling skills, good passing ability, anaifanya timu icheze kwa kuunganisha team members kufanya shambulio.
Kuna tofauti ya kimajukumu inayotofautisha kati ya midfielders na playmakers.
Midfielder huwa analimitiwa na position yake, anacheza eneo husika kwenye pitch iwe nyuma ya washambuliaji ama eneo la mbele la mabeki. Wakati Playmaker ni yule mchezaji mwenye uwezo wake binafsi, ikiwa na maana kwamba playmaking ni ule ubora wa mchezaji binafsi (individual quality). Playmaker anaplan mchezo mzima kwa vision na passing ability yake na kutengeneza nafasi kwa wengine kuattack.
Playmaker anahitaji kuwa na skills zifuatazo:
Passing skills ( pass ndefu na fupi).
Ball control skills, uwezo mzuri wa kukaa na kutembea na mpira.
Dribbling skills, uwezo mkubwa wa kukimbia na mpira mguuni.
Off the ball position intelligence, ufahamu wa kukaa eneo sahihi wakati akiwa hana mpira.
1v2 Possession, playmaker anatakiwa awe mzuri pale ambapo kunakuwa hakuna nafasi nyingine inabidi awe na uwezo wa kuwatoka wapinzani...
The switch up, awe mzuri kwenye suala la kubadilisha upande kutoka eneo moja la uwanja hadi mwingine..
Technical and Ball control + vision, ajue kuisaidia timu kwa kuwachezesha team members kwa kuwapush kwenda mbele kufanya shambulizi.
Kwa maana hiyo pale Chelsea FC tuna deep lying playmaker type kutokana na mfumo unaotumika wa 3421, Jorginho ndiye controler akichezesha timu kuanzia eneo la dimba la chini.
Hakim Ziyech pia ni play maker mzuri hasa alipokuwa akicheza Ajax, ila kwa pale CFC hajapewa majukumu hayo labda kutokana na mfumo uliopo.
Pia timu inaweza kucheza na multiple playmakers, kucheza na playmaker zaidi ya mmoja kunaifanya timu iwe hatari zaidi.