Mayagillah Sports Fact

Mayagillah Sports Fact Tanzania Sports Pundit

MALENGO YA YANGA KUIDHOHOFISHA SIMBA YALIFANIKIWAUkiangalia namna YANGA walivyochanga karata zao vizuri  juu ya kuhakiki...
26/03/2023

MALENGO YA YANGA KUIDHOHOFISHA SIMBA YALIFANIKIWA

Ukiangalia namna YANGA walivyochanga karata zao vizuri juu ya kuhakikisha simba inadhohofika ni kumchukua MB3 Bernard Morrison.

Ipo hivi BM alipokuwa Simba alikuwa ana uwezo wa kuwasaidia timu kupata matokeo wakati wowote hasa pale timu ilipoonekana kuna ugumu wa kupata matokeo na alifanya hivyo kwenye michezo mingi tu na hata uwepo wake pale bench ulikuwa unaleta tumaini kuwa nje yupo mtu ambae akiingia anaweza kufanya kitu kisichotarajiwa wakati wowote.

Na hii ilikuwa tishio sana kwa wapinzani wanapokutana na Simba ikiwa BM3 ameanza au akiwa bench kiasi kwamba ikapelekea mabosi wa jangwani kumvuta pale Avic Town lakini mkakati mkubwa ulikuwa ni kuifanya Simba ikose huduma yake japokuwa kiuhalisia hakukuwa na uhitaji wa muhimu sana katika kikosi cha yanga cha sasa ndiomana hata k**a hayupo pengo lake halionekani.

YANGA imefanikiwa katika hili


Mayagillah Sports Fact

22/09/2022

TBT Nakumbuka siku hii nilikuwa nazungumzia mchezo mgumu na wa mwisho ugenini kwa upande wa Mbeya City Vs Yanga na game ilichezwa tarehe 25/06/2022 ik**alizika kwa sare ya kufungana

UKWELI ULIVYOJuma Mgunda katika njia za Pitso MosimaneImekuwa ni desturi yetu sisi watanzania kubeza watu wetu kwa kuona...
22/09/2022

UKWELI ULIVYO

Juma Mgunda katika njia za Pitso Mosimane

Imekuwa ni desturi yetu sisi watanzania kubeza watu wetu kwa kuona hawana ubora, lakini tupo tayari kuimba majina ya wageni hata k**a uwezo wao ni wa kawaida kabisa katika soka letu kwakuwa tu bado tunaandamwa na jinamizi la kasumba ya kuamini mgeni pekee ndio anaweza kufanya mambo makubwa katika soka letu (ni utumwa wa kifikra tu) hususa ni katika hizi timu kubwa jambo ambalo linazika vipaji vingi na uwezo wa wazawa wengi katika soka letu.

Ipo hivi, tunalalamika sana kwamba hatuna makocha wengi wazawa lakini ukweli ni kwamba uhaba wa makocha wazawa unachagizwa na dhihak, kejeli na dharau kwa mashabiki na baadhi ya wadau wa soka

Kivipi, lilipoibuka suala la JUMA MGUNDA kuhusishwa na klabu ya SIMBA hii ilikuwa ni neema kubwa sana katika soka letu la Tanzania lakini kwa bahati mbaya bila ya tafiti za kina baadhi ya wadau na mashabiki walikuwa mstari wa mbele kukosoa kwamba Mgunda hastahili kuwa kucha wa Simba wa muda wakiamini kwamba haendani nayo na wengine walidai hana vyeti, na wengine waliamini Simba ndio mwisho wao hatua za awali kwakuwa katika benchi kwenye mechi ya mashindano ya CAF imeongozwa na Mtanzania.

Ukweli ulivyo, Uwepo wa Mgunda pale Simba ni tiba kubwa katika fikra za wadau wengi wa soka ambao wanaamini katika wageni na hata wageni wanaposhindwa kufanya vizuri basi wanaamini wazawa wana msaada tu wakati wa matatizo (migogoro)tu lakini katika kipindi cha neema klabuni basi wageni ndio wapewe timu.

Juma Mgunda katika njia za Pitso Mosimane naamini k**a Simba watamuamini Mgunda na kumuachia timu k**a kocha wa kudumu Mgunda atakwenda kuwa kocha mkubwa barani Afrika k**a ilivyokuwa kwa Pitso Mosimane na hata Ibenge, pale Simba pana kila aina ya facilities zitakazo msaidia Mgunda k**a Kocha mkuu kwani wachezaji wa kushindana CAF wapo na timu inajimudu hivyo kwake itakuwa ni rahisi sana kuonesha kile kitu alichonacho kutokana na taaluma yake ya ukocha. Naamini Mgunda ni Pitso wa Tanzania kwani ameshaweza kuprove mambo mengi sana kwa ligi ya ndani na ameweza kusumbua vichwa makocha wa timu kubwa hapa nchini kwa kuwafunga na hata kutoa sare.

K**a Simba wataendelea kumuamini na timu ikafanya vizuri katika mashindano haya ya klabu bingwa naamini JUMA MGUNDA anakwenda kutambulika Afrika kwa haraka sana kwanza kupitia bland ya timu anayoifundisha katika soka la Afrika inafatiliwa sana kwasasa hivyo sitoshangaa kumuona klabu kubwa katika maeneo mengine ya Afrika baada ya kuondoka Simba hapo baadae. Ikumbukwe hata Pitso Mosimane amekuwa kocha mkubwa Barani Afrika baada ya kuaminika na klabu kubwa nchini kwao ya Mamelod hvyo hata njia hii ya Mgunda ni k**a njia ile ya Pitso Mosimane.

Karibu, follow, share, like na comment kwa taarifa za ukweli na uhakika

Enjoy soccer na Mayagillah sports fact

UKWELI MTUPUUkitazama kwa makini kwenye mchezo wa soccer utagundua kuwa uwekezaji ndio silaha kubwa katika maendeleo ya ...
17/09/2022

UKWELI MTUPU

Ukitazama kwa makini kwenye mchezo wa soccer utagundua kuwa uwekezaji ndio silaha kubwa katika maendeleo ya mchezo huu, silaha ambayo ndio nguzo kuu katika mafanikio ya vilabu na hata timu za taifa. Leo hii tunapomuona Yanga SC kapangwa na Zalan FCkutoka Sudan kusini wapo watu wanaodhami kuwa Yanga kapangiwa kibonde au hastahili kucheza nae lakini sio kweli, ila quality ya kikosi cha yanga ni matokeo ya silaha kubwa katika soccer ambayo ni uwekezaji chini ya muwekezaji wao (GSM).

Leo hii Yanga inakwenda katika mkondo wa pili wakiwa na faida ya goli 4 sio jambo dogo hata kidogo hii inadhihirisha kuwa ule uwekezaji uliokwenda kufanyika ndani ya klabu hiyo haya ndio matokeo yake, sajili zilizofanyika, maandalizi, morali ya wachezaji, utulivu wa benchi la ufundi sambamba na support kubwa kutoka kwa mashabiki wao ndio vitu vinavyochagiza mafanikio ya timu yao na ndio siri pekee inayofanya Yanga SC kuwa bora zaid hivi karibuni.

Tulizoea kuona kwa miaka kadhaa iyopita namna vilabu vyetu vilivyokuwa vikitazamwa k**a inavyo tazamwa Zalan FC (Under dog) leo hii, lakini kupitia uwekezaji taratibu tunaanza kuhama kutoka huko walipo wakina Zalan FC tunasogea mbele kuwakuta walipo wakina AS Vita, Tp Mazembe. Nafikiri huu ndio wakati sahihi wa kuchagua upande mwingine uliobora katika viunga vya soka kuliko ule upande dhaifu wa (Under dog) na hakika taratibu soka letu litazidi kuwa bora barani Afrika.

KUMBUKA:

Hakuna mchawi katika soka bali siri ya mafanikio ipo katika uwekezaji tu....

Karibu like, comment, share page yetu na endelea kufatilia taarifa zetu za uchambuzi wa kina hapahapa

Mayagillah Sports Fact

"Kikubwa ni kuendelea kupambana ili tupate matokeo na kuingia kwenye hatua inayofata. Taratibu tutakuwa tunaelekea kweny...
17/09/2022

"Kikubwa ni kuendelea kupambana ili tupate matokeo na kuingia kwenye hatua inayofata. Taratibu tutakuwa tunaelekea kwenye malengo yetu."

"Natoa shukrani zangu (kwa mashabiki), kwenye mechi ya kesho tutaenda kupambana kwa ajili yao, kwa ajili ya mashabiki, viongozi na hata sisi sababu mpira ndio maisha yetu."

"Kikubwa tunachozungumza ni kutengeneza kitu kimoja, utamaduni wa klabu, malengo ya klabu kwa msimu husika. Simba ni timu ya mataji lakini pia timu ya mafanikio."- Nahodha msaidizi wa klabu ya Simba Mohamed Hussein

Karibu like, comment na share page yetu kwa taarifa za kina na uchambuzi wa uhakika hapahapa
Mayagillah Sports Fact

"Tunajua kwamba klabu imetupa malengo yake hivyo kwetu kwa pamoja tunatakiwa kufika pale. Tupo tayari kufikia malengo ya...
17/09/2022

"Tunajua kwamba klabu imetupa malengo yake hivyo kwetu kwa pamoja tunatakiwa kufika pale. Tupo tayari kufikia malengo ya klabu."

"Kwa ujumla ni kwamba mimi pamoja na benchi la ufundi maandalizi ya mchezo wa kesho yamekamilika. Tuwaombee vijana walale salama na kesho waamke salama kwenda kukamilisha wajibu wao."

"Binadamu anajifunza kwa makosa (ilivyokuwa msimu uliopita), mechi inakwisha mpaka filimbi ya mwisho. Mechi ya kwanza Malawi ilikuwa kipindi cha kwanza, wachezaji wanatambua hilo, wapo tayari kupambana."

"Wachezaji wote wapo tayari, atakayepewa gwanda la Simba kesho naamini ataiwakilisha vyema."

"Mafanikio yote mazuri sio ya mtu mmoja. Muunganiko niliokuta, umoja ulipo, ari iliyopo kwa wachezaji na ahadi waliyonipa siku ya kwanza, wachezaji wanajua jukumu lao naamini watafanya vizuri."

"Tumejiandaa kiufundi kwenda kushindana."- Kocha Mkuu wa Simba Juma Mgunda

Address

Dar Es Salaam
KIGAMBONI

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mayagillah Sports Fact posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Mayagillah Sports Fact:

Share

Category